Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Katavi
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman
Kinana amewasili mkoani Katavi kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi
itakayokwenda sambambamba na kupokea taarifa na kukagua miradi ya
maendeleo.
Katika ziara hiyo ya kikazi ameongazana na Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka na baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege Katavi Kinana amepokelewa na Wana CCM Mkoa wa
Katavi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Beda Katani.
Baada
ya kuwasili Kinana akiwa na Shaka wamepata nafasi ya kusailiamana na
wanachama wa Chama hicho na kisha kupokea taarifa ya CCM na Serikali
Mkoa wa Katavi.
Akipokea taarifa hiyo Kinana ameelezwa hali ya
mwenendo wa Chama na Serikali na kwa sehemu kubwa ameambiwa hali ni
shwari na kwamba viongozi wamekuwa na ushirikiano mkubwa hali
inayofanywa utekelezaji wa Ilani kufanyika kwa kiwango cha kuridhisha.
Kwa
mujibu wa ratiba Kinana ambaye ameanza ziara leo Julai 25 ,2022 akiwa
mkoani hapa mbali ya kupokea taarifa ya Chama na Serikali atazindua
mradi wa fremu 15 za biashara, pia atatembelea mradi wa fremu za vibanda
188.
Aidha Kinana atazindua kituo cha afya na kuzungumza na
wananchi na wanachama, pia baadae atazungumza na WanaCCM na viongozi
mbalimbali . Kinana atakuwa katika ziara ya mikoa ya Nyanda za Juu
ukiwemo Mkoa wa Katavi na kisha kuelekea Mkoa Rukwa, Songwe na Mbeya.Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman
Kinana akiwa katika picha mbalimbali akisaliamia na wana CCM mkoa wa
Katavi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Katavi kwa ajili ya
kuanza ziara ya kikazi sambamba na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama
hicho.PICHA NA MICHUZI JR-KATAVI
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Abdulrahaman Kinana akisailiamiana na viongozi wa
Chama na Serikali mkoa wa Katavi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa
Mpanda kwa ajil ya kuanza ziara mkoani humoMatukio
mbalimbali katika picha baada ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara
Abdulrahman Kinana kuwasili uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi kwa
ajili ya kuanza ziara ya kikazi
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndugu Abdulrahman
Kinana akisaliamiana na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Katavi
baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Mpanda kwa ajili ya kuanza
ziara ya kikazi
No comments:
Post a Comment