KILOLE MZEE BLOG

KILOLE MZEE BLOG

A great place to access the latest news and information.

BREAKING NEWS

Wednesday, November 24, 2021

SIMBA YAANZA KUIWINDA RED ARROWS

11:41 AM 0

 

Na: mwandishi wetu

KIKOSI cha simba leo kimeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Kombe la  shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows Kutoka Zambia.

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Arrow utachezwa Novemba 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni.

Hata hivyo kikosi kicho kinaingia uwanjani kikiwa na morali  baada ya kuwa ba kocha mpya ambaye ameiwezesha simba kupata ushindi dhidi ya Ruvu shooting katika ligi ya NBC.

Kikosi hicho kimerejea katika uwanja wao wa Bunju baadabya kufanyiwa matengenezo katika eneo la kuchezea(pitch).

Tangu kuanza kwa msimu huu tinu imekuwa inafanya mazoezi katika uwanja wa Boko Veteran kwa ajili ya kupisha matengenezo hayo ambayo tayari yamekamilika na kikosi kimerejea rasmi Nyumbani.

Read More

RAIS SAMIA AMELETA NEEMA KWA JAMII

11:41 AM 0

 Na Mwandishi wetu Mihambwe


Miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa nchi nzima imeleta neema na unafuu mkubwa kwa jamii.

Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu wakati alipofanya ziara ya kawaida ya ukaguzi wa miradi wa maendeleo ya Elimu ya ustawi wa jamii kwa Taifa dhidi ya mapambano ya Uviko 19 ambapo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta neema kubwa kwa Watanzania kupitia miradi hiyo.

"Miradi hii ya Elimu si tu inaenda kupunguza tatizo la uhaba wa vyumba vya madarasa bali pia inawaimarisha Wananchi kiuchumi. Mathalani kuna Mafundi viongozi na Masaidia wamepata kazi za ujenzi,wanaingiza fedha; Kuna Wafanyabiashara, Wasafirishaji, Wauzaji vifaa vya ujenzi madukani, Wauzaji vifaa vya kujengea kama vile mawe, kokoto, mchanga nk hawa wote wamepata neema ama fursa ya kufanya biashara, kujiongezea kipato kupitia utekelezaji ujenzi miradi hii ya Elimu na mengineyo. Hivyo kwa niaba ya Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe tunamshukuru sana Rais Samia kwa miradi hii inayoenda kuondoa uhaba wa Madarasa na pia amefanya mzunguko wa fedha uongezeke kwa jamii ambapo miradi hiyo inatekelezwa." Alisema Gavana Shilatu.

Gavana Shilatu pia alitumia ziara hiyo kuwasisitiza Mafundi kuongeza kasi zaidi ya ujenzi, kamati za miradi kuhakikisha wanasimamia ubora wa vifaa na ujenzi ili miradi ikamilike kwa wakati, kwa ubora unaolingana na thamani ya fedha.

Tarafa ya Mihambwe imepata fedha toka Serikali kuu Tsh. Milioni 420 kujenga vyumba vya Madarasa 19 kwa shule za Sekondari 5 na vyumba Madarasa 2 kwa shule Shikizi moja. Katika fedha hizo hizo pia wanajenga ofisi 9 za Waalimu na kuweka viti na meza kwenye Madarasa hayo yote 21.Read More

WANANCHI NALASI MASHARIKI KUWASHIWA UMEME WA REA

11:39 AM 0

 

Kazi ya kuchimba mashimo kwa ajili ya kusimika nguzo za umeme ikiendelea katika kijiji cha Likuyu Mandela, wilayani Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma, wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy


Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Pili wilayani Namtumbo (kushoto) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini Wakili Julius Kalolo (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy (kofia nyeusi), walipokuwa kwenye ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini


Mwenyekiti wa Kijiji cha Chilundundu Kusini, Adolphina Ndomba (wa kwanza-kushoto) na Kaimu Katibu Tarafa, Kata ya Nalasi Mashariki, Salumu Kijumu (wa pili-kushoto) wakizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo (wa pili-kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (wa kwanza-kulia). Viongozi wa REA walikuwa katika ziara ya kazi wilayani Tunduru

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo na Ujumbe aliofuatana nao, wakiangalia uharibifu wa miundombinu ya umeme katika maeneo tofauti wilayani Tunduru na Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma, walipokuwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati vijijiniNguzo zikiwa zimeharibiwa kwa kuchomwa moto katika maeneo tofauti wilayani Tunduru na Namtumbo, Mkoa wa Rukwa. Taswira hizi zilichukuliwa wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo (wa tatu-kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy (wa tatu-kulia) pamoja na Ujumbe waliofuatana nao wakati wa ziara kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini wilayani Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma

…………………………………………………………………

Na Veronica Simba, REA – TUNDURU

Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili katika kijiji cha Nalasi wilayani Tunduru, Mkoa wa Ruvuma, yuko katika hatua za mwisho kukamilisha upelekaji umeme katika kijiji hicho ili wananchi waunganishiwe na kuanza kunufaika na nishati hiyo.

Hayo yalibainika wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Wakili Julius Kalolo aliyefuatana na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy, kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini wilayani Tunduru, Novemba 23, 2021.

Wakizungumza na Uongozi wa Kata ya Nalasi Mashariki na wa Kijiji cha Chilundundu Kusini, viongozi hao wa REA walisema baada ya kufanya ukaguzi na kuzungumza na Mkandarasi, wamejiridhisha kuwa umeme utawashwa Nalasi ndani ya muda mfupi ujao.

Hivyo, waliwaomba viongozi wa Kata ya Nalasi kufikisha salamu zao kwa wananchi na kuwahamasisha kukamilisha maandalizi katika nyumba zao tayari kuupokea umeme.

Aidha, walimwagiza mwakilishi wa Mkandarasi ambaye ni muunganiko wa kampuni mbili za Guangdong Jianneng Electric Power Engineering Co. LTD na White City International Contractors LTD, kuhakikisha anakamilisha mapema iwezekanavyo, ujengaji wa miundombinu na kuwasha umeme ili kukidhi kiu ya muda mrefu ya wananchi wa Nalasi.

Katika hatua nyingine, viongozi hao wa REA waliwaasa wananchi kutunza miundombinu ya umeme inayopita katika maeneo yao ili kuepusha hasara kubwa inayopatikana kwa serikali na wananchi wenyewe pindi kunapotokea uharibifu wake.

“Serikali inatumia fedha nyingi sana kufikisha miundombinu ya umeme vijijini ili kuwaletea maendeleo wananchi, hivyo inapoharibiwa ni hasara kubwa siyo kwa serikali tu, bali pia na kwa wananchi wenyewe wa eneo husika,” alifafanua Mwenyekiti wa Bodi Wakili Kalolo.

Alisema kwamba yeyé pamoja na Ujumbe aliofuatana nao katika ziara hiyo wamesikitishwa kuona uharibifu wa miundombinu ya umeme katika maeneo kadhaa na kueleza kuwa hali hiyo inatokea katika maeneo tofauti tofauti kote nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Saidy alisema uharibifu unaofanywa iwe ni kwa kudhamiria au kwa bahati mbaya unapaswa kuwekewa mikakati ya kuuzuia usiendelee kutokea ili kulinda miundombinu husika.

Akifafanua, alisema hilo linawezekana kwa viongozi katika maeneo mbalimbali kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hiyo kwa kushirikiana na kupeana taarifa.

Vilevile, Wakili Kalolo na Mhandisi Saidy waliwaelekeza viongozi wa Nalasi kuwatahadharisha wananchi kujiepusha na vishoka ambao wamekuwa wakiwatapeli wananchi katika maeneo mbalimbali ambako miradi ya umeme vijijini inatekelezwa.

Walisema, Nalasi inaweza kukumbwa na wimbi hilo la vishoka kama ilivyo katika maeneo mengine yaliyofikiwa na umeme ambapo matapeli hao hutumia mwanya wa uhitaji mkubwa wa wananchi kuunganishiwa umeme kutekeleza vitendo vyao vya kitapeli.

“Wengi watakuja na kujitambulisha kwenu kama wafanyakazi wa REA na TANESCO, wapeni tahadhari wananchi ili wawe waangalifu,” alisisitiza Mhandisi Saidy.

Aidha, waliwaelekeza viongozi wa Nalasi kuwakumbusha wananchi kuwa hivi sasa malipo yote ya serikali yanafanywa kupitia lipa namba hivyo wasikubali kulipa pesa taslimu kwa mtu yeyote na kupewa risiti.

Viongozi hao walitoa maelekezo kwa TANESCO ngazi ya Mkoa kufika Nalasi mara moja kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna bora ya kujiandaa kuupokea umeme, kutunza miundombinu na kuepuka matapeli.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini na Mkurugenzi Mkuu wa REA wako katika ziara ya kazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi na Pwani.
Read More

NHC YATAKIWA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI

11:38 AM 0

 Na Munir Shemweta, MISENYI


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuendelea kuwekeza miradi ya kimkakati itakayoliwezesha shirika kujiongezea kipato.

Dkt Mabula ametoa kauli hiyo tarehe 23 Novemba 2021 wakati akikagua mradi wa jengo la kibiashara la NHC lilipo mpakani mwa Tanzania na Uganda eneo la Mutukula wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.

Naibu Waziri ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili mkoani Kagera alisema, ilichofanya NHC kujenga jengo la kibiashara katika mpaka wa Tanzania na Uganda Mutukula ndicho serikali inachokitaka pale inapokuwa na taasisi zinazojitegemea katika uendeshaji pia ziwe na njia tofauti za kujiongezea kipato kitakachosaidia kuongeza miradi mingine.

" Hiki ambacho NHC mmekifanya hapa kujenga jengo la biashara Mutukula ndicho inachokitaka serikali kuwa inapokuwa na taasisi inayojitegemea kiuendeshaji pia iwe na njia tofauti za kujiongezea kipato cha shirika " alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Dkt Mabuka, mradi wa jengo la biashara Mutukula unatoa fursa kwa wafanyabiashra kutoka nchi jirani ya Uganda kuja Tanzania kununua bidhaa kwani awali ilikuwa aibu kuona wafanyabiashara wakienda kununua bidhaa katika maduka ya nchi hiyo.

" Ilikuwa aibu tunaenda upande wa pili kununua bidhaa lakini sasa na wao waje hapa kufanya biashara na hii ni alama tosha kuwa tunaanza kubadilika" alisema Naibu Waziri Mabula.

Aidha, Dkt Mabula aliongeza kuwa, ana imani mradi wa jengo la kibiashara Mutukula ukienda vizuri eneo lingine linalokusudiwa kujenga maduka litapata msaada wa fedha za ndani zitakazopatikana kupitia mradi huo.

Naibu Waziri Mabula aliongeza kuwa, ni kweli wafanyabiashara wadogo wamachinga hawawezi kupanga katika jengo la mradi huo lakini shirika linaweza kujenga maduka kuzunguka jengo hilo yanayoweza kubadilisha sura ya eneo kuonesha kuwa eneo hilo limepangwa na isiwe viduka visivyoonesha tofauti kati ya eneo lilipangwa na lisilopangwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Projestus Tegamaisho Mutukula amelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa uamuzi wake wa kuwekeza mradi huo katika eneo la Mutukula ambapo aliiomba NHC kuangalia uwezekano wa kuwekeza mradi kama huo katika mji unaopanuka wa Bunazi wilayani Misenyi.

"Niwashukuru NHC kwa kutuwekea kitega uchumi cha jengo hili na tunaomba mtujengee jengo lingine katika mji wa Bunazi ili maeneo ya Misenyi yawe na uwelezaji mkubwa" alisema Tegamaisho.

Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kagera Maneno Mahenge alisema, mradi wa jengo la Mutukula kwa sasa umefikia asilimia 99 na mradi huo umetumia asilimia 50 tu ya eneo lake lenye ukubwa wa mita za mraba 7900.

" Tunataka mradi huu wa kitega uchumi hapa Mutukula uwe shopping centre area inayotembelewa na wananchi wengi wakiwemo wa nchi jirani ya Uganda na jengo hili tayari lina wapangaji 36" alisema Mahenge.

Aidha, katika kuhakikisha NHC unawekeza majengo ya kimkakati maeneo ya mipakani Meneja huyo wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kagera alieleza kuwa, tayari amepeleka Andiko Makao Makuu ya NHC kwa ajili ya kuanzisha miradi kama wa Mutukula katika eneo la Rusumo mpaka wa Tanzania na Rwanda pamoja na Kabanga katika mpaka wa Tanzania na Burundi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia sehemu ya Jengo la Kibiashara la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo Mutukula wilayani Misenyi mkoani Kagera alipokwenda kukagua mradi wa jengo hilo tarehe 23 Novemba 2021

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kagera Maneno Mahenge (Kulia) alipokwenda kukagua Jengo la Kibiashara la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika eneo la Mutukula wilayani Misenyi mkoani Kagera tarehe 23 Novemba 2021.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifurahia bidhaa aliyonunua kwenye moja ya maduka yaliyopanga katika jengo la Kibiashara la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo Mutukula wilayani Misenyi mkoani Kagera alipokwenda kukagua mradi wa jengo hilo tarehe 23 Novemba 2021.

Sehemu ya ndani ya Jengo la Kibiashara la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo Mutukula wilayani Misenyi mkoa wa Kagera.
Read More

Ndumbaro Asitisha Zuio La Kusafirishwa Bidhaa Ghafi Za Misitu Nje

11:37 AM 0

 Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amaeondoa zuio la usafirishaji bidhaa ghafi za misitu kwa masharti ikiwemo ‘veener’ na utomvu kutoka miti ya misindano kwenda nje ya nchi mpaka mwezi wa sita mwakani yaani 2022 na kuruhusu kontena 187 zilizopo bandari kusafirishwa na kontena zilizopo nje ya bandari zifuate utaratibu uliowekwa na Wizara ili zipate kibali cha kusafirishwa.

Akizungumza kwenye kikao kilichoratibiwa na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) Jijini Dar es Salaam, Dkt. Ndumbaro amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Sita ni kuona sekta ya misitu inatoa mchango stahiki kwenye pato la taifa na kuwataka wadau kujiandaa na utekelezaji wa maazimio yaliyopitishwa kwenye kikao kilichowakutanisha wadau hao Novemba 15 mwaka huu Wilayani Mafinga.

“Malengo ya serikali ni kuona sekta ya misitu inaleta tija kwa wazalishaji wake. Nyinyi kama wadau hamna budi kujiandaa kutekeleza maagizo ya serikali ambayo na ndiyo maana nimetoa zuio nililoliweka ili mupate muda wa kujiandaa,’’ alisema Dkt. Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro alisisitiza kuwa, “Katika kipindi hiki cha mpito mpaka kufikia mwezi juni mwakani vibali vyote vitatolewa na Waziri kwa kufuata masharti yakiwemo kuleta taarifa za kodi, taarifa za haki za wafanyakazi, thamani halisi ya mzigo pamoja na kuwa na mpango kazi wa kampuni wa kuleta mashine haraka.

Aidha, Dkt.Ndumbaro aliwataka wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla kukubaliana na mabadiliko ambayo ndiyo msingi wa maendeleo katika jamii yoyote duniani hivyo amehimiza jamii kuwa katika mtazamo chanya katika kupokea mabadiliko.

“Serikali imefanya tafiti na kujiridhisha kuwa faida inayopatikana katika kusafirisha malighafi ni ndogo hivyo ili kukuza kipato kupitia sekta ya misitu imeamua kuzuia usafirishaji wa mazao hayo na kuhimiza uwekazaji utakaotoa bidhaa ya mwisho na kwenda sokoni,’’ alisema Dkt.Ndumbaro.

Aliongezea kuwa serikali itaendelea kupaanua wigo na kutoa fursa zaidi za uwekezaji na ajira nchini kwani kwa kufanya zuio hilo kutachochea uwekezaji wa viwanda vikubwa hapa nchini jambo litakalozalisha ajira na kukuza pato la taifa.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa TNBC Dkt. Godwill Wanga mbali ya kumshukuru Waziri kwa kuja kuzungumza na wadau wa misitu, amewataka wadau hao kuwa na imani na serikali, kwani imefanya maboresho hayo ili sekta hiyo iwe na tija kwa wazalishaji na kuchangia kwenye pato la taifa.

“Kwa muda mrefu sasa sekta ya misitu imeonekana ikitoa mchango mdogo kwenye pato la taifa, kwa kuliona hilo serikali imekuja na maazimio haya ikiwa ni hatua ya kuifanya sekta hii iwe na tija sio tu kwa wazalishaji bali hata kwa uchumi wa nchi”, alisema Dkt. Wanga.

Dkt. Wanga aliongeza kuwa, “Sekta hii inahitaji tafiti nyingi ili wadau wajue fursa nyingi zaidi zilizopo, ambazo tukizutumia vyema itakuwa lulu kwa taifa.’’

Naye Mwenyekiti Mwenza wa kikundi kazi cha Misitu TNBC, Bw. Ben Sulus mbali ya kumpongeza Dkt. Ndumbaro kwa kutenga muda kuja kuwasikiliza wadau hao, amewataka wadau hao kubadilika na kuendana na matakwa ya serikali kwa kuwekeza zaidi kwenye kuleta mitambo na kuanzisha viwanda vingi nchini ili uzalishaji ufanyike hapahapa jambo ambalo litatengeneza fursa kubwa za ajira kwa watanzania.

“Sisi kama sekta binanfsi tujipange vizuri kwa kujiandaa kutekeleza kipindi hiki mpaka kufikia mwakani, tuweze kuanzisha viwanda vingi nchini vitakavyozalisha ajira kwa vijana wetu wengi zaidi”, alisema Bw. Sulus.

Waziri Dkt. Ndumbaro aliahidi kukutana tena na wadau wa sekta ya misitu tarehe 13 na 14 mwezi dssemba mwaka huu Jijini Arusha ili kuzungumza nao sambamba kuangalia namna utekelezaji wa maagizo ya serikali unavyofanyika.

Read More

RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA TAASISI ZA FEDHA NCHINI

11:36 AM 0

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua mkutano wa 20 wa Taasisi za Fedha nchini utakaofanyika jijini Dodoma, tarehe 25 na 26 Novemba 2021, utakaojadili uimarishaji wa uchumi wa Tanzania kufuatia janga la UVIKO-19.

Mkutano huo, ambao umeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mabenki nchini (TBA), unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki takribani 300 kutoka taasisi za fedha, sekta binafsi, serikali, mashirika ya kimataifa, taasisi za elimu, asasi za kiraia na vyombo vya habari.

Mada nne zitawasilishwa na wataalam waliobobea kutoka ndani na nje ya nchi, ambazo ni:

∙ Ukuaji wa uchumi endelevu wakati na baada ya janga la UVIKO -19: Vipaumbele na sera mbadala;

∙ Kuchochea kasi ya maendeleo ya kidijitali katika kuimarisha ukuaji endelevu wa uchumi;

∙ Sarafu za kidijitali: Uzoefu, vihatarishi na usimamizi; na

∙ Kuongeza mikopo kwa sekta binafsi baada ya janga la UVIKO-19: Wajibu wa Serikali, taasisi za fedha na sekta binafsi.

Mada hizo zimechaguliwa kuendana na hali ya sasa, ambapo uchumi wa dunia unaendelea kuimarika kufuatia athari za janga la UVIKO-19, na kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia za kidijitali na fedha za mtandaoni.

Mikutano ya Taasisi za Fedha ilianzishwa na Benki Kuu ya Tanzania mwaka 1980 na imekuwa ikifanyika kila baada ya miaka miwili. Mkutano wa 19 wa Taasisi za Fedha ulifanyika jijini Dar es Salaam mwezi Novemba 2019.

Imetolewa na :

Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki

 BENKI KUU YA TANZANIA
Read More

Tuesday, November 23, 2021

Benki Ya Exim Yakabidhi Msaada Wa Madawati 100 Kwa Ajili Ya Mkoa Wa Mwanza

11:31 AM 0

 


Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (katikati) sambamba na viongozi waandamizi wa benki ya Exim akiwemo Mkuu wa Idara ya Rasimimali watu wa benki hiyo Bw Fredrick Kanga (Kulia- walioketi) na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano kutoka Benki ya Exim, Stanley Kafu (kushoto- walioketi) wakiwa wameketi katika moja ya madawati 100 yaliyotolewa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya Mkoa wa Mwanza yakiwa ni sehemu kampeni ya ugawaji madawati 1000 yaliyofadhiliwa na benki hiyo kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali nchini. Wengine ni maofisa waandamizi wa elimi kutoka mkoa huo.


Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (Kulia) akipokea msaada wa madawati 100 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano kutoka Benki ya Exim, Stanley Kafu (kushoto) kwa ajili ya kusaidia kuondoa adha ya upungufu wa mawadati katika Shule mbalimbali za Msingi mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa ugawaji wa madawati 1000 katika mikoa mbalimbalimbali hapa nchini kupitia mpango wake wa kusaidia jamii ujulikanao kama Exim Cares.


Sehemu ya madawati 100 yaliyotolewa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya Mkoa wa Mwanza yakiwa ni sehemu kampeni ya ugawaji madawati 1000 yaliyofadhiliwa na benki hiyo kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali nchini.


Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (kushoto) akijipongeza na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi Veronica Kessy wakati wa hafla ya makabidhiano madawati 100 yaliyotolewa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya Mkoa wa Mwanza yakiwa ni sehemu kampeni ya ugawaji madawati 1000 yaliyofadhiliwa na benki hiyo kwa ajili ya shule za msingi katika mikoa mbalimbali nchini.

Read More