WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameitaka
CitiBank kuharakisha mchakato wa kuifanyia Tanzania tathimini ya uwezo
wake wa kukopa na kurejesha mikopo (credit rating) ili iweze kuyafikia
masoko ya kimataifa yanayotoa mikopo kwa gharama nafuu.

Dkt.
Nchemba alitoa rai hiyo Jijini Washington DC, Marekani, baada ya
kukutana na uongozi wa Benki hiyo pamoja na Benki ya Mitsubish ya Japan,
ambayo pia imeonesha nia ya kuiwezesha Tanzania kupata mikopo
itakayosaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
Alisema
kuwa Serikali iliahidi bungeni wakati wa Bajeti Kuu ya Serikali ya
Mwaka 2021/2022 kwamba ingefanyiwa tathimini kuhusu uwezo wake wa kukopa
na kulipa madeni na kuitaka Citibank na washirika wake kukamilisha kazi
hiyo kabla ya mwezi Julai mwaka huu.
Dkt.
Nchemba alisema kuwa Ukamilishwaji wa zoezi hilo utasaidia nchi kuweza
kuyafikia masoko mbalimbali ya fedha duniani kwa gharama nafuu na
kuongeza imani ya wawekezaji kwenda kuwekeza teknolojia na mitaji
nchini.

Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar Mhe. Saada Mkuya
Salum (Mb), akizungumza jambo wakati ujumbe wa Tanzania ulipokutana na
kufanya mazungumzo uongozi wa Benki ya Mitsubish ya Japan, kwenye Ofisi
za Ubalozi wa Tanzania, jijini Washinton DC, Marekani. Kushoto ni Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).

Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kushoto), ukiwa katika picha ya pamoja na
Ujumbe kutoka Benki ya Mitsubish ya Japan, katika Ofisi za Ubalozi wa
Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani. Wa pili kushoto ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar Mhe. Saada Mkuya Salum
(Mb), wa nne kulia ni Kiongozi wa Ujumbe wa Benki ya Mitsubish ya Japan,
Bw. Christopher Marks.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango - Zanzibar,
Mhe. Saada Mkuya Salum, alisema kuwa mazungumzo yao na Benki ya
Mitsubish ya Japan yalikuwa na mafanikio makubwa ambapo Benki hiyo
imeahidi kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia mikopo ya kibiashara
lakini yenye masharti nafuu.
Alisema
kuwa mikopo hiyo imelenga kuharakisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya
kimkakati inayoendelea kutekelezwa nchini pamoja na miradi mipya
itakayoombewa fedha ili kuharakisha utekelezaji wake kwa manufaa ya
nchi.
Alitolea
mfano wa mahitaji ya Zanzibar ya kutekeleza mpango wa uchumi wa buluu
pamoja na ujenzi wa miundombinu itakayosaidia kuchochea maendeleo ya
wananchi ikiwemo ujenzi wa bandari, viwanja vya ndege, barabara, nishati
ya umeme, kuimarisha sekta ya utalii na masuala ya uvuvi.

Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kushoto), ukiwa katika picha ya pamoja na
Ujumbe kutoka Benki ya Mitsubish ya Japan, katika Ofisi za Ubalozi wa
Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani. Wa nne kulia ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar Mhe. Saada Mkuya Salum
(Mb). Wa pili kulia ni Kiongozi wa Ujumbe wa Citibank, Bw. Peter
Sullivan. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha
na Mipango-Washington DC).
Wakizungumza
katika mikutano hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Citibank Bw. Peter
Sullivan, pamoja na Kiongozi wa Ujumbe wa Benki ya Mitsubish ya Japan
Bw. Christopher Marks, waliahidi kuwa watahakikisha Tanzania inafikia
malengo yake ya kujitathimini lakini pia kupata mikopo nafuu ya
kutekeleza program mbalimbali za miradi ya maendeleo.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, anaongoza ujumbe
wa Tanzania kwenye mikutano ya Majira ya Kipupwe inayoendelea mjini
Washington DC, Marekani ambapo pamoja na mikutano hiyo ya kawaida,
ujumbe huo unakutana na taasisi na mashirika mbalimbali yanayoonesha nia
ya kuwekeza fedha zao nchini Tanzania
No comments:
Post a Comment