Mke
wa Rais wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha
Bora, Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na viongozi wa Mkoa wa Kusini
Wilaya ya Kati Unguja baada ya kuwasili katika viwanja vya Skuli ya
Msingi Uzi,kwa ajili ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wazee kuazia umri wa
miaka 70 wa Shehia mbili za Uzi na Ngambwa na (kushoto kwake) Mkuu wa
Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Rashid Hadidi.(Picha na Ikulu).
Mke
wa Rais wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha
Bora, Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi mmoja wa Wazee wa Kijiji cha Uzi
Sadaka ya Futari, aliyokabidhi kwa Wazee wa Shehia mbili za Uzi na
Ngambwa , hafla hiyo iliyofanyika katika Skuli ya Msingi Uzi Wilaya ya
Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu).
Mke
wa Rais wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha
Bora, Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi Misahafu Sheikh Ali Othman kwa
ajili ya Madrasa na Misikiti ya Shehia ya Uzi na Ngambwa, hafla hiyo
iliyofanyika katika Skuli ya Msingi Uzi.(Picha na Ikulu).
Mke
wa Rais wa Zanzibar ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha
Bora, Mama Mariam Mwinyi akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wananchi
wa Uzi, wakati wa hafla ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wazee wa umri wa
miaka 70, hafla hiyo iliyofanyika katika Skuli ya Msingi Uzi na (kushoto
kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadidi.(Picha na
Ikulu).
No comments:
Post a Comment