BENKI
ya Standard Chattered imeihakikishia Tanzania kuwa iko tayari kutoa
fedha zaidi kwenye miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali
ikiwemo Reli ya kisasa ya SGR na ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya
ndege.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa
tatu kushoto), na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-
Zanzibar Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) (wa pili kushoto), wakiwa katika
picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya Standard Chertered, baada ya
kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa
Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu Mtendaji wa Standerd Cheretered-Tanzania Bw. Sanjay Raghani, Katibu
Mkuu, Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil, Mwenyekiti wa
Standard Chertered, Bw. Jose Vinals.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)
(katikatiwa), na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-
Zanzibar Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) (wa tano kushoto), wakiwa katika
picha ya pamoja na Uongozi wa Benki ya Standard Chertered Pamoja na
Ujumbe wa Tanzania, baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika
Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani. Ahadi
hiyo imetolewa na Uongozi wa Benki hiyo ukjongozwa na Mwenyekiti wake
Bw. Jose Vinals, ulipokutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa
Tanzania, ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu
Lameck Nchemba (Mb). kando ya mikutano ya majira ya kipupwe ya Benki ya
Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Jijini
Washington DC, Marekani.
Akizungumza
baada ya kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa
Tanzania, Washington DC, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu
Nchemba alisema kuwa Benki hiyo ilitoa mkopo unaotumika kujenga reli ya
kisasa ya SGR kutoka Morogoro hadi Makutupora, mkoani Singida, na kwamba
hivi sasa Serikali iko kwenye mazungumzo na Benki hiyo ili itoe mkopo
mwingine kwa ajili ya vipande vingine vya reli hiyo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)
(kulia), akisalimiana na Mwenyekiti wa Benki ya Standard Chertered
duniani Bw. Jose Vinals, baada ya kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika
Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)
(kulia), na Mwenyekiti wa Benki ya Standard Chertered Bw. Jose Vinals,
wakibadilishana kadi za mawasiliano baada ya kumalizika kwa mkutano wao
kuhusu uwekezaji kwenye miradi ya kimkakati nchini Tanzania, uliofanyika
Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango- Zanzibar Mhe. Saada
Mkuya Salum (Mb), akisalimiana na Mwenyekiti wa Benki ya Standard
Chertered Bw. Jose Vinals, baada ya kumalizika kwa majadiliano kati ya
Ujumbe wa Tanzania na Benki hiyo kuhusu upatikanaji wa mikopo kwa ajili
ya ujenzi wa miradi uliofanyika Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington
DC, Marekani.Kwa
upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar
Mheshimiwa Saada Mkuya Salum, alisema kuwa katika kuimarisha shughuli za
utalii na kukuza uchumi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepanga
kuboresha miundombinu ya Uwanja wa Ndege wa Pemba na kwamba mazungumzo
yanayoendelea kati ya Serikali na Benki hiyo yatawezesha kupata fedha
kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Akizungumza
kwa niaba ya Uongozi wa Standard Chartered baada ya kumalizika kwa
mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki hiyo nchini Tanzania Bw.
Sanjay Rughani, alisema kuwa wako tayari kutoa fedha zaidi kwa ajili ya
miradi iliyowasilishwa na Serikali kwenye Benki hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango- Zanzibar Mhe. Saada
Mkuya Salum (Mb), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Standard
Chertered – Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, baada ya kumalizika kwa
majadiliano kati ya Ujumbe wa Tanzania na Benki hiyo kuhusu upatikanaji
wa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo, uliofanyika katika
Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb),
akizungumza jambo wakati wa kikao kati ya ujumbe wa Tanzania na Ujumbe
wa Benki ya Standard Chertered kuhusu upatikanaji wa rasilimali fedha
kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati nchini Tanzania. Mkutano huo
umefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Washington DC, Marekani.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Benki hiyo duniani Bw. Jose Vinals.(Picha na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango-Washington
DC, Marekani).Alisema kuwa pamoja na ahadi ya kutoa
fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kimkakati inayotekelezwa na
Serikali, Benki hiyo pia iko tayari kuwashawishi wawekezaji wengine
kutoka maeneo mbalimbali duniani kwenda kuwekeza mitaji na teknolojia
nchini Tanzania.
Ikumbukwe
kwamba Benki ya Standard Chartered, tarehe 13 Februari, 2020, iliipatia
Tanzania mkopo wenye thamani ya dola za Marekani, bilioni 1.5 kwa ajili
ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha kuanzia Morogoro hadi
Makutupora, mkoani Singida.
No comments:
Post a Comment