WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amemuagiza Katibu Mkuu
anayesimamia Sekta ya Mifugo kumsimamisha kazi mkandarasi anayejenga
miundombinu ya mnada wa Ndelema wilayani Handeni mkoani Tanga kwa
kushindwa kufanya kazi kwa wakati.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (Mb) akiongea na moja ya
familia katika Kijiji cha Msomera wakati alipotembela kijijini hapo
kukagua kazi ya maandalizi ya kuwapokea wafugaji kutoka kwenye Hifadhi
ya Ngorongoro inayoendelea kufanyika. Mhe. Ndaki amewasihi kuwapokea
wafugaji wanaokuja vizuri na kuishi nao.
Waziri
Ndaki ametoa agizo hilo Aprili 23, 2022 baada ya kukagua kazi
iliyofanyika katika ujenzi wa miundombinu ya mnada huo ambapo wakati
anapita kukagua hakukuwa na kazi yoyote inayoendelea na mkandarasi
hakuwepo kwenye eneo la ujenzi.
Pamoja
na agizo hilo la kusitisha mkataba wa mkandarasi huyo, Waziri Ndaki pia
ameagiza kusitishwa kwa malipo ambayo yalikuwa yapo kwenye mchakato kwa
kuwa mkandarasi huyo hastahili kulipwa kutokana na kazi aliyoifanya.
Aidha, amemuagiza Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Mifugo kumtafuta
mkandarasi mwingine mwenye uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa wakati ndani
ya siku 14 ili kazi hiyo iweze kuendelea.
Waziri
Ndaki amesema serikali ilishatenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha
miundombinu ya mnada huo inajengwa kwa lengo la kuwezeshwa wafugaji
kuuza mifugo yao kwenye mazingira mazuri na kusaidia katika kuongeza
ukusanyaji wa maduhuli. Hivyo amewasihi wakandarasi kuhakikisha
wanafanyakazi zao kwa wakati kulingana na mikataba kwani serikali
haitamvumilia mkandarasi mzembe.

Naye
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Siriel Mchemba amesema kuwa mnada huo
ni muhimu sana katika ukusanyaji wa maduhuli ya halmashauri hivyo
ucheleweshwaji wa ujenzi wa miundombinu yake unakwamisha maendeleo ya
mji wa handeni ambayo yangepatikana kupitia fedha ambazo zingekusanywa
hapo.
Prof.
Hezron Nonga ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Mifugo, amesema
kuwa mkandarasi huyo alishaandikiwa barua ya onyo kutokana na
ucheleweshaji wake wa kazi lakini pia alishaitwa wizarani kwa lengo la
kumtaka amalize kazi aliyopewa ya ujenzi wa miundombinu kwenye mnada wa
Ndelema.

Katika
ziara yake hiyo, Waziri Ndaki alitembelea Kijiji cha Msomera wilayani
Handeni mkoa wa Tanga kukagua kazi zinazoendelea kufanyika kwa ajili ya
maandalizi ya kuwapokea wafugaji kutoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro
wakati alipotembelea Kijiji cha Msomera wilayani Handeni.
Waziri Ndaki amewasihi wafugaji hao kuhamia kwenye Kijiji hicho kwa kuwa mazingira yanayoandaliwa na serikali ni mazuri kwa shughuli zao za mifugo.

No comments:
Post a Comment