Mfuko
wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa elimu ya Hifadhi ya Jamii
kwa baadhi ya wasanii ambao ni washindi wa Tuzo za Muziki Tanzania
kuhusu umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na
baadaye.
Baada
ya elimu hiyo wasanii hao walipata fursa ya kujiunga na NSSF ikiwa ni
utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na
Michezo kupitia kwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye
aliahidi kuwa Wizara pamoja na kutoa zawadi kwa wasanii walioshinda
vilevile Wizara iliona ni vema kuwalipia NSSF wasanii hao ambao
wameshinda kwa kipindi cha mwaka mmoja na baadaye wataendelea wenyewe.
Meneja
Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele alieleza umuhimu wa
wasanii kujiunga, kuchangia ili wajiweke akiba kwa maisha yao ya sasa
baadaye ambapo pindi watakapokosa kipato waweze kunufaika na mafao
mbalimbali ikiwemo pensheni ya uzee.
Naye,
Abdulaziz Abeid ambaye ni Afisa Matekelezo Mkuu wa Sekta Isiyo Rasmi
alisema Mfuko umeweka mifumo rahisi na rafiki kwa kila Mtanzania
aliyejiajiri mwenyewe kujiwekea akiba. Hivyo alitoa wito kwa wasanii
kuchangamkia fursa hiyo.
Kwa
upande wake, Mratibu wa Tuzo za Muziki kutoka BASATA, Mrisho Mrisho,
aliwataka wasanii kujiunga na NSSF kwa ajili ya kujiwekea akiba ya
maisha ya baadaye kwani kuna faida nyingi ambazo watanufaika nazo.
Msanii
wa muziki wa singeli, ambaye alichukua Tuzo ya Mwanamuziki bora wa
Singeli kwa wasanii wanawake, Snura Mushi, aliishukuru NSSF kwa
kuwafikia wasanii ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao
ya sasa na baadaye.
Naye,
mkali wa singeli, Sholo Mwamba aliipongeza NSSF kwa kuwafikia wasanii
na kuwaomba wasanii wengine ambao hawajashinda kuchangamkia fursa hiyo
ya kujiunga na NSSF kwani ni Mfuko wenye faida kubwa sana.
Meneja
Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele, akitoa mada kuhusu
umuhimu wa kujiwekea akiba kwa baadhi ya wasanii walioshinda Tuzo za
Tanzania Music Award. Ambapo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
ilitoa zawadi mbalimbali kwa wasanii walioshinda ikiwepo zawadi ya
kuwachangia NSSF na NHIF katika kipindi cha mwaka mmoja na baada ya hapo
wasanii wenyewe wataendelea kuchangia..jpeg)
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Matiko Mniko,
akitoa neno la utangulizi wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa baadhi
ya wasanii washindi wa Tuzo za Muziki Tanzania kuhusu elimu ya Hifadhi
ya Jamii kwa upande wa NSSF na Bima ya Afya (NHIF).
Afisa
Matekelezo Mkuu wa Sekta Isiyo Rasmi, Abdulaziz Abeid akitoa mada kwa
baadhi ya wasanii washindi wa Tuzo za Muziki Tanzania kuhusu umuhimu wa
kujiunga, kuchangia ili wajiwekea akiba kwa maisha yao ya sasa na
baadaye.
Msanii
wa Muziki, Snura Mushi ambaye ni mmoja wa mshindi kwenye Tuzo za Muziki
Tanzania akiuliza maswali mbalimbali kuhusu NSSF mara baada ya mada
zilizotolewa na NSSF kwenye Semina ya kuwaongezea uelewa wa Hifadhi ya
Jamii iliyoandaliwa na BASATA.



Baadhi
ya maofisa wa NSSF wakijibu maswali mbalimbali kutoka kwa baadhi ya
wasani walioshinda Tuzo za Muziki Tanzania mara baada ya kupata elimu ya
Hifadhi ya Jamii ili waweze kujiunga na kujiwekea akiba kwa maisha yao
ya sasa na baadaye.
Meneja
Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akifuatilia jinsi
wasani Snura Mushi na Sholo Mwaba wakijaza fomu za kujiunga na NSSF,
ambapo mwaka huu katika Tuzo za Wanamuziki Bora wasanii hao walikuwa
miongoni mwa wasanii bora.jpeg)







Baadhi
ya Wafanyakazi wa NSSF wakiwasaidia wasanii kujaza fomu za kujiunga na
NSSF ambapo Wizara itawalipia michango ya mwaka mmoja na baada ya hapo
wasanii hao wataendelea kuchangia wenyewe
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, April 22, 2022
Wasanii washindi wa Tuzo za Muziki Tanzania wapata elimu na kujiunga na NSSF
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment