Kiongozi
wa Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi.
Mercy Amani (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada kwa Mkuu wa Shule ya
Msingi Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango (kulia) uliotolewa na
Wafanyakazi Wanawake wa TTCL kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa
Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni
juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za
kundi hilo maalum.
Mmoja
wa wakilishi wa Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania
(TTCL), akikabidhi sehemu ya msaada kwa Afisa Elimu Maalum Jiji Dar es
Salaam, Bw. Swalehe Msechu (kulia) uliotolewa na Wafanyakazi Wanawake wa
TTCL kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru
Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni juhudi za kuisaidia
jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za kundi hilo maalum.
Kiongozi
wa Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi.
Mercy Amani (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada kwa Mkuu wa Shule ya
Msingi Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango (kulia) uliotolewa na
Wafanyakazi Wanawake wa TTCL kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa
Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni
juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za
kundi hilo maalum.
Mkuu
wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango
(aliyesimama) akizungumza kuwakaribisha baadhi ya Wafanyakazi Wanawake
wa Shirika la TTCL walipowasilisha msaada wao kwa Wanafunzi wenye
mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es
Salaam jana ikiwa ni juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali
kutatua changamoto za kundi hilo maalum. Kulia ni Kiongozi wa Wanawake
Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Mercy Amani
na viongozi waalikwa wakifuatilia.
Na Mwandhishi Wetu
WAFANYAKAZI
Wanawake toka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wametoa msaada kwa
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam
wenye mahitaji maalum ikiwa ni juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na
Serikali kulisahidiakundi hilo lenye uhitaji.
Msaada
huo wa vyakula kama unga wa mahindi, mchele, mafuta ya kula, sukari,
chumvi, sabuni pamoja na taulo za kike kwa watoto wahitaji umekabidhiwa
jana shuleni hapo na baadhi ya wafanyakazi wanawake kutoka TTCL.
Akizungumza
Kiongozi wa Wanawake wa TTCL, Kiongozi wa Wanawake Makao Makuu TTCL,
Bi. Mercy Amani alisema akinamama hao wameguswa na changamoto
wanazozipata wanafunzi wenye mahitaji maalum hivyo kuamua kujitolea kwa
kuchangishana wao wenyewe na baadaye juhudi zao kuungwa mkono na
menejimenti ya TTCL.
Aidha
alisema TTCL inaungana na kuwashukuru wazazi, walezi, ndugu, jamaa
pamoja na Serikali kwa ujumla kwa kile kuwawezesha kundi hilo maalum la
watoto kupata elimu yao shuleni hapo. Aliongeza kuwa watoto hao wanaweza
kufanya makubwa endapo watapata elimu yao vizuri.
Aidha,
TTCL inashukuru sana kwa fursa hii mliyotupa sisi Wafanyakazi Wanawake
wachache kwa niaba ya wenzetu walioko nchi nzima, kuja kuwaona watoto na
kuwapatia zawadi na msaada wetu ndogo pamoja na kuwafadhili.
Picha
ya pamoja kati ya baadhi ya Wafanyakazi Wanawake Makao Makuu ya Shirika
la Mawasiliano Tanzania (TTCL) pamoja na sehemu ya viongozi na
Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya
jijini Dar es Salaam walioshiriki hafla ya makabidhiano ya msaada kwa
Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya
jijini Dar es Salaam jana uliotolewa na TTCL ikiwa ni juhudi za
kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za kundi hilo
maalum.
Pamoja
na hayo, Bi. Amani aliwashukuru uongozi wa shule kwa juhudi mbalimbali
wanazoziweka katika kuhakikisha watoto hawa hao wanajifunza masomo
darasani na kushiriki shughuli anuai za kijamii ikiwemo michezo, hali
ambayo huwajenga kiafya pia.
"Taarifa
zimetuonesha kuwa hii ni shule nzuri, yenye juhudi kubwa ya kuwalea
vijana na kufanikisha ndoto zao za kitaaluma na ki maisha kwa ujumla.
Hapa ni mahali pazuri ambapo raia wema na nguvu kazi ya nchi hii kwa
siku zijazo zinaandaliwa. Hii ndio sababu ya sisi pia kuguswa na kuomba
kuja kuwatembelea," alisema Bi. Amani.
Hata
hivyo, aliwataka wanafunzi hao kutumia kikamilifu nafasi ya kupata
elimu walioipata iwe chachu ya kufanya vizuri zaidi, na kamwe changamoto
za kimaumbile na miundombinu zisiwafanye kukata tamaa bali iwe ari ya
kusoma kwa bidii na kuzingatia yale yanayofundishwa na walimu na walezi
na hatimaye kuzifikia ndoto zao.
TTCL
ina majukumu na malengo ya kutoa huduma bora ya Mawasilino ndani na nje
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia inayo kampuni tanzu ya T- PESA
ambayo inatoa huduma ya fedha mtandao, ambayo inawawezesha Wananchi
kupata huduma mbalimbali kama Kutuma Fedha, Kulipia Ankara za huduma
kama vile Maji, Umeme (LUKU), Ving’amuzi (Visimbuzi) na Kununua
vifurushi vya TTCL huku huduma nyingine zikiendelea kuongezwa.
Naomba
nitoe rai yangu kwenu, tuoneshe uzalendo wetu kwa kutumia bidhaa za
TTCL ambazo kwa hakika ni mali halisi ya Watanzania kwa 100%. Tumia
chako. Jenga kwako. RUDI NYUMBANI.
Kiongozi
wa Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi.
Mercy Amani (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada kwa Mkuu wa Shule ya
Msingi Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango (kulia) uliotolewa na
Wafanyakazi Wanawake wa TTCL kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa
Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni
juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za
kundi hilo maalum.
No comments:
Post a Comment