Afisa
kinga kutoka shirika hilo wa mkoa wa Mbeya Bi,Damali Lucas akieleza
namna mradi wao unavyofanya kazi na kuisadia jamii katika maswala mbali
mbali.
Baadhi ya wateja wakipata maelezo katika banda la Walter Reed
Dr.Cassian
Nyandindi ni kamishna msaidizi kutoka mamlaka ya kudhibiti na kupambana
na madawa ya kulevya akitoa wito kwa jamii kutoa taarifa juu watumiaji
wa dawa ya kulevya ili waweze kusaidiwa.
Baadhi
ya waelimishaji wakiwa katika banda kwa ajili ya kupokea wateja na
kuelimisha juu maswala mbalimbali ikiwemo virusi vya ukimwi na madawa ya
kulevya.
Na Amiri Kilagalila,Njombe
KATIKA
kuunga mkono juhudi za serikali ili kuhamasisha jamii kuelewa na
kupokea chanjo ya Corona katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa
huo,shirika lisilo la kiserikali la HJFMRI limetumia kikamilifu maonesho
katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe kwa kutoa elimu dhidi ya chanjo
hiyo.
Akizungumza
na vyombo vya habari katika banda lao lililopo katika uwanja huo
utakapofanyika uzinduzi wa mbio za Mwenge kitaifa,Afisa kinga kutoka
shirika hilo wa mkoa wa Mbeya Bi,Damali Lucas amesema jukumu lao kubwa
nikuunga mkono serikali katika mapambano hayo.
“Kwa
kushirikiana na mkoa wa Njombe tumekuja kusaidia kuunga mkono juhudi za
serikali katika kuhamasisha jamii kwenye maswala ya chanjo dhidi ya
Uviko-19 kwa kuwa sisi ni miongoni mwa watu ambao tumechanja ili
kujikinga na hata walengwa wote ambao tumekuja nao wote
wamekwishachanja”alisema Damil Lucas
Aidha
amesema shirika hilo kupitia Walter Reed wanatekeleza pia mradi
unaohusika na kukinga maambukizi ya virusi vya ukimwi na kutoa afua
mbali mbali katika jamii ili kuendelea kukinga maambukizi ya virusi vya
Ukimwi huku pia wakisaidia waraibu wa dawa za kulevya na kubainisha kuwa
walengwa wao katika shirika hilo wapepatachanjo ya Corona ili kujikinga
na maambukizi.
Boaz
Tweve kutoka Rukwa na Sad Juma kutoka Mbeya ni miongoni mwa watu
wanaofanya kazi na shirika hilo katika kuhamasisha na kushawishi wateja
ikiwemo kupima virusi vya Ukimwi na kuanza kupata huduma za dawa
wanasema wanatumia nafasi zao pia kuhamasisha chanjo ya Corona ili
kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi.
Dr.Cassian
Nyandindi ni kamishna msaidizi kutoka mamlaka ya kudhibiti nan a
kupambana na madawa ya kulevya amesema kupitia mbio za Mwenge wanatoa
ujumbe na kuelemisha jamii juu ya madhara ya dawa za kulevya yakiwemo
madhara ya kiuchumi na afya lakini kwa mwaka huu wamekuwa wakizungumzia
maswala ya Corona.
“Kupitia
mbio za Mwenge kwa mwaka huu tunazungumzia swala zima la maambukizi ya
Corona na kupokea chanjo,mapambano ni muhimu na ninapenda kuhamasisha
umma kupambana dhidi ya Uviko-19 “Dr.Cassian Nyandindi ni kamishna
msaidizi kutoka mamlaka ya kudhibiti nan a kupambana na madawa ya
kulevya
Aidha ametoa wito kwa jamii kutoa taarifa juu ya watumiaji wa dawa za kulevya ili waweze kupata huduma.
Mbio
za mwenge zinatarajiwa kuzinduliwa leo mkoani Njombe katika uwanja wa
sabasaba mjini Njombe na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.Philip Mpango.
No comments:
Post a Comment