KIKOSI
cha KMC FC leo kimefanya maandalizi yake ya mwisho kuelekea katika
mchezo wake wa Ligi kuu ya NBC Soka Tanzania Bara dhidi ya Namungo ya
Ruangwa Mkoani Lindi utakaopigwa hapo kesho katika Uwanja wa Uhuru hapa
jijini Dar es Salaam saa 16:00 jioni.
Kwa
mujibu wa barua iliyotumwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB, ilieleza
kwamba mchezo huo utapigwa siku ya MAJIya Aprili tatu mwaka huu katika
uwanja huo wa Uhuru badala ya Azam Complex Chamanzi kama ratiba ya awali
ilivyoelekeza kutokana na kukamilika kwa matengenezo yaliyokuwa
yakifanyika katika uwanja huo.
Kutokana
na barua hiyo ya TPLB, Timu ya Manispaa ya Kinondoni inarejea sasa
katika uwanja wake wa nyumbani ikiwa ni baada ya kupita kwa takribani
michezo mitano ikicheza nje ya uwanja huo na hivyo kulazimika kutumia
uwanja wa Azam Complex Chamanzi ambapo mara ya mwisho kutumia uwanja huo
wa Uhuru ilikuwa ni kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Azam
FC na KMC kupata ushindi wa magoli mawili kwa moja.
KMC
FC chini ya Kocha Mkuu Thierry Hitimana hadi sasa imejiandaa vema kweye
mchezo huo licha ya kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba Timu ya
Namungo imekuwa ikifanya vizuri katika michezo yake lakini ubora wa
wachezaji pamoja na Benchi zima la ufundi litahakikisha kuwa alama tatu
muhimu zinapatikana.
“Tumetoka
kupoteza michezo miwili mfululizo, na tunakwenda kwenye mchezo mwingine
tukiwa nyumbani, hii ninafasi kwetu ya kusahihisha makosa ya awali na
kwamba Kocha Mkuu Hitimana katika kipindi hiki ambacho Timu zilikuwa
kwenye mapumziko kupisha kalenda ya FIFA amefanya maboresho kwenye
maeneo ambayo aliona yanachangamoto ambazo zilikosesha Timu kupata
matokeo mazuri, hivyo mashabiki zetu watarajie kupata burudani.
Kwakipindi
kirefu hatujatumia uwanja wetu halisi wa nyumbani, na sasa tunarejea
kwenye mchezo dhidi ya Namungo, hivyo Tunaipongeza TPLB kwa ushirikiano
mkubwa waliotuonesha kwa kipindi chote hicho na sasa tunakwenda kesho
tukifahamu kabisa mchezo utakuwa mgumu lakini KMC FC tumejipanga
kuondoka na alama tatu muhimu.
Aidha
Klabu ya KMC FC inawasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi siku ya kesho
kwenye mchezo huo muhimu ambao wachezaji wamejiandaa vizuri kuhakikisha
kwamba wanatoa burudani iliyoambatana na ushindi, ukizingatia kuwa
itakuwa siku ya wekeand.
No comments:
Post a Comment