Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu
amewataka watanzania wanaotumia usafiri wa bodaboda kuwa makini ili
kupunguza ajali zinazopelekea kupoteza viungo vya mwili.
Ameyasema
hayo leo Machi 21, 2022 Wakati akifungua mafunzo ya wataalamu wa
upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo pamoja na wagonjwa mahututi
yanayofanyika katika taasisi ya mifupa ya MOI jijini Dar es Salaam.
Waziri
Ummy amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati, kwa sababu Tanzania
inashuhudia ongezeko la upasuaji wa mifupa, uti wa mgongo pamoja na
magonjwa ya mishipa ya fahamu kutokana na ajali mbalimbali ikiwa ni
pamoja na bodaboda.
"Sio jambo jema kwa Bodaboda kuanza kujifunza
kuendesha pikipiki leo na kesho anaingia barabarani kuchukua abiria,
ajali nyingi zinasababishwa na uzembe na kutofuata sheria za
barabarani". Amesema Waziri Ummy.
"Tutakaa na wenzetu wa Wizara
ya mambo ya ndani kuhakikisha tunatafuta ufumbuzi wa hili ili kupunguza
ajali za uzembe zinazoweza kuepukika kwa kuwa watu wengi wamekuwa
wakipoteza viungo vyao vya mwili kwa kuvunjika na kuwekewa vya bandia."
Amesema Waziri Ummy.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na watanzania kwa
kushirikiana na wataalamu kutoka nchini Marekani, Australia pamoja na
Canada na lengo la mafunzo hayo ni kuongeza ujuzi, uzoefu na utaalamu.
Katika
hatua nyingine Waziri Ummy ameendelea kuwasihi watanzania kujitokeza
kupata chanjo ya UVIKO-19 kwa kuwa bado Corona ipo Tanzania.
Pia
amesema shirika la Afya Duniani limethibitisha kuwa kuna kirusi kipya
cha Corona kimegundulika ambacho Delta kimechanganyana na Omicron na
kinatambulika kwa jina la Omicron.DA1
"Serikali imeshachukua
hatua za kuendelea kuchunguza na kujua kwamba kimeingia Tanzania au bado
lakini nchi nyingine tayari wameshathibitisha." Amesema Waziri Ummy.
Hivyo
amewata watanzania kuendelea kuchukua tahadhari kama wanavyoelekeza
wataalamu ikiwepo kunawa mikono kwa maji tiririka na kuvaa barakoa.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, March 21, 2022
WAZIRI UMMY AMESEMA AJALI NYINGI ZA BODABODA ZIMECHANGIA WATU KUPOTEZA VIUNGO VYAO
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment