Katika Kipindi cha mwaka mmoja
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
kumekuwa na mafanikio ya kiongozi wa kusimamia utendaji na kufanikiwa
kuvutia wawekezaji kwa wingi nchini ikiwemo sekta ya madini.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Mhe.Nape Nnauye ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya kuchambua
kurasa za siku 365 za Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan katika
kongamano iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es
Salaam.
Mhe. Waziri ameipongeza STAMICO kwa kuwa na mafanikio
yanayooneka kwa kipindi kifupi sana na kuitaka kuendeleza mafanikio
hayo yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu
ya Sita ikiwani sehemu ya kuendeleza mazuri yote yaliyoachwa na uongozi
wa awamu tano zilizopita na amerekebisha maeneo yenye makosa kwa lengo
la kukuza uchumi wa nchi na kuondoa utegemezi.
Akizungumzia
Mafanikio ya Shirika Bw. Deusdedith Magala kwa niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika hilo Dkt. Vanance Mwasse amesema, katika mwaka mmoja
au siku 365 za Mama, STAMICO imefanikiwa kuongeza mapato ya ndani na
kwa kuanza kujiendesha kwa faida. Pia ni katika awamu ya sita ambapo kwa
mara ya kwanza Shirika limeweza kutoa gawio Serikalini.
Aidha,
Bw. Magala ameeleza mafanikio ni pamoja na ujenzi na ufunguzi wa kiwanda
kikubwa cha kusafisha madini ya dhahabu cha Mwanza Precious Metals
Refinery chenye uwezo wa kusafisha kilo 480 za dhahabu kwa siku kwa
kiwango cha kimataifa cha asilimia 99.99.
Aidha Bw. Magala
amesema Shirika limeweza kununua mitambo ya kisasa nane (8) ya
uchorongaji yenye thamani ya Bilioni 11.2 na vilevile tumeweza kupata
kandarasi za uchorongaji zenye jumla ya shilingi bilioni 33 katika
migodi mikubwa kama GGM, Buckreef na Buhemba ukilinganisha kandarasi
zenye thamani ya Shilingi bilioni 17 za mwaka uliopita.
Bw.
Magala ameainisha mafanikio mengine yakiwemo kuanzisha mradi wa
kutengeza mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe (Coal Briquttes).
Kuboresha vituo vya mfano vya wachimbaji wadogo na kuwaunganisha na
taasisi za kibenki ili waweze kukopesheka pamoja na maboresho makubwa
yaliyofanyika kwenye Vituo vya Mfano vya Lwamgasa, Katente na Itumbi.
Pia
Shirika limesaini mikataba na benki za CRDB, NMB na KCB ili kuanza
kuwakopesha wachimbaji wadogo walikuwa hawaaminiwi kukopeshwa. Pia
Shirika limesaini makubaliano na GST ili kushirikiana kuainisha maeneo
yanayofaa kwa kuwapa wachimbaji wadogo. Sambamba na hilo, Shirika
linaagiza mashine tano za Uchorongaji kwa ajili ya kuwasaidia wachimbaji
wadogo.
Hafla hiyo iliyobebwa na kauli mbiu isemayo " Mama yuko
Kazini", imewakutanisha wadau kutoka Wizara na taasisi mbalimbali ambazo
zilipata fursa ya kueleza jinsi zilivyofanikiwa ndani ya kipindi cha
mwaka mmoja wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.
No comments:
Post a Comment