Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema baada ya
kupokea taarifa ya Kamati ya Kitaifa iliyochunguza uchafuzi wa mazingira
uliojitokeza hivi karibuni ndani ya Mto Mara, ameagiza timu ya
wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kushirikiana na Wizara ya Maji
na Wizara ya Mifugo kuipitia kwa kina taarifa hiyo na kuwasilisha
uchambuzi wa kitaalamu pamoja na Mpango kazi wa utekelezaji.
Ameyasema
hayo leo tarehe 21 Machi 2022 jijini Dodoma mara baada ya kukutana na
waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi kuhusu ripoti iliyowasilishwa
kwake na Kamati ya Kitaifa iliyochunguza uchafuzi wa mazingira mwishoni
mwa wiki.
Amewataka watanzania kuwa watulivu na kuepusha
taharuki inayoendelea mitandaoni kwani azma ya Serikali ni kulinda afya
ya wananchi wake. Pia, ameagiza ripoti hiyo ya wataalamu itafsiriwe kwa
lugha ya Kiswahili na kusambazwa kwa umma ili maudhui yake yaweze
kufahamika kwa jamii.
Kuhusu taarifa ya awali ya uchunguzi wa
kimaabara iliyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Dkt. Jafo
amesema taarifa hiyo ndio ilipelekea kuundwa kwa Kamati ya kuchunguza
kwa kina chanzo cha uwepo wa kiwango cha mafuta na kukosekana kwa hewa
ya oksijeni, ambapo imebainika kuwa taarifa hiyo haikinzani na ile ya
Timu ya Kitaifa
Aidha, Dkt. Jafo amesema anakaribisha na kupokea
ushauri na maoni mbalimbali kutoka kwa wadau na wataalamu wa mazingira
wa namna bora ya kutatua changamoto za mazingira nchini.
Machi
12, 2022 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. Dkt. Selemani Jafo aliunda Kamati ya Kitaifa yenye wajumbe 11
kuchunguza chanzo cha uchafuzi wa mazingira uliojitokeza ndani ya Mto
Mara chini ya uenyekiti wa Prof. Samwel Manyele wa Idara ya Uhandisi wa
Kemikali na Madini kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kamati
iliyowasilisha taarifa yake 19 Machi 2022.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo (katikati) akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma
leo tarehe 21/03/2022 na kufafanua kuhusu taarifa ya Kamati ya Kitaifa
iliyochunguza uchafuzi wa mazingira uliojitokeza ndani ya Mto Mara.
Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt.
Andrew Komba, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bw. Edward Nyamanga,
Mkurugenzi Mkuu Baraza la Tafa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka na Mkurugenzi Msaidizi – Idara ya Mazingira
Bw. Faraja Ngerageza.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, March 21, 2022
DKT. JAFO AWATAKA WATANZANIA KUONDOA TAHARUKI
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment