WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema wakulima 2,409 na Vyama vya Ushirika
vitano wamewezeshwa kukopa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 28.2
kupitia hatimiliki za ardhi zilizotolewa na Mpango wa Kurasimisha
Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).
Baadhi
ya watumishi wa MKURABITA wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama
(hayupo pichani) wakati ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi hao.
Mhe.
Jenista amesema hayo jijini Dodoma, wakati akizungumza na watumishi wa
MKURABITA alipofanya ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza
uwajibikaji kwa watumishi hao.
Mhe.
Jenista amesema kuwa, mikopo hiyo imewawezesha wakulima hao kuingia
kwenye kilimo bora na cha kisasa ambacho kinaliwezesha taifa kuwa na
akiba ya hifadhi ya chakula cha kutosha.
“Mikopo
hiyo imewasaidia pia wakulima kuondokana na ukulima wa kawaida na
kuingia kwenye kilimo cha biashara ambapo anakuwa ni mlipa kodi mzuri
anayechangia ukuaji wa uchumi,” Mhe. Jenista amefafanua.
Mhe.
Jenista ameongeza kuwa, wamiliki 206 waliorasimisha viwanja maeneo ya
mjini wametumia hatimiliki kupata mikopo yenye thamani ya zaidi ya
shilingi bilioni 3.
Akimkaribisha
Mhe. Waziri kuzungumza na watumishi, Mratibu wa MKURABITA Dkt. Seraphia
Mgembe amesema wakulima hao 2409 waliotumia Hatimiliki za ardhi kupata
mikopo ya kiasi cha shilingi bilioni 28.2 wamethibitisha wenyewe kwa
maandishi kupitia fomu walizojaza.
Aidha,
Dkt. Mgembe amesema, wafanyabiashara waliopata mafunzo kupitia
MKURABITA wameweza kukopa zaidi ya shilingi bilioni 9.38 kwa ajili ya
kuongeza mitaji ya biashara zao.
No comments:
Post a Comment