RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameziagiza
Wizara za Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa
kushirikiana na Wizara ya Afya kuhakikisha kuwepo mifumo madhubuti ya
kutambua mapema aina mbalimbali za ulemavu ili kuweza kutoa huduma
ipasavyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea Tuzo ya Pongezi kutoka kwa Watu wenye Ulemavu Tanzania kutoka
kwa Stella Jailos wa SWAUTA kabla ya kuzungumza na Makundi hayo Ikulu
Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Machi, 2022.
Rais
Samia ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na watu wenye ulemavu
katika hafla iliyofanyika viwanja vya Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.
Mhe.
Rais Samia amesema unyanyapaa wa watu wenye ulemavu katika jamii
umepungua kutokana na jitihada za baadhi ya watu wenye ulemavu kupaza
sauti, hivyo kuwataka watu wenye ulemavu kujikubali walivyo katika
jamii.
Makundi mbalimbali ya burudani ya Watu wenye Ulemavu wakitoa burudani
katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 16 Machi,
2022.
Kwa
upande wa elimu, Serikali imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa elimu
kwa watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya awali hadi Chuo Kikuu.
Kwa
mwaka 2022, jumla ya watoto wenye ulemavu 2,883 wameandikishwa katika
Elimu ya awali, wakiwemo wavulana 1,470 na wasichana 1413 huku wanafunzi
1,157 wakiandikishwa kidato cha kwanza.
Makundi mbalimbali ya watu wenye Ulemavu, Sauti ya Wanawake wenye
Ulemavu (SWAUTA), Shirikisho la Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu Zanzibar
(SHIJUWAZA) na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu SHIVYAWATA,
wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan wakati akiwahutubia katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani
Dodoma leo tarehe 16 Machi, 2022. (Picha na Ikulu).
Vilevile,
Rais Samia amesema Serikali inafanya jitihada kuimarisha hospitali na
kuajiri madaktari bingwa kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye vichwa
vikubwa na kuwataka wananchi kuwafichua watoto hao mapema ili waweze
kupatiwa tiba ya upasuaji.
Halikadhalika,
Rais Samia ametoa rai kwa watu wenye ulemavu kujitokeza kuhesabiwa
wakati wa Sensa ya Watu na Makazi mwezi Agosti mwaka huu wa 2022 bila
kuwaficha watoto wenye ulemavu ili kupata takwimu sahihi zitakazowezesha
Serikali kupanga mipango ya maendeleo shirikishi kwa watu wenye
ulemavu.
No comments:
Post a Comment