Wananchi wa kata ya Olmoti
Wilayani Arumeru Mkoani Arusha wamepatiwa elimu ya utunzaji wa mazingira
ikiwa pamoja na kuotesha miti katika maeneo yao ikiwa ni kupambana na
ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo
yamebainishwa na mratibu wa zoezi la utoaji elimu ya upandaji miti na
mazingira kutoka Club ya utunzaji mazingira (Lions club) Chief Masanya
Kabena wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kwa Wananchi wa vijiji
vya kata hiyo.
Amesema maeneo mengi ya jamii ya wafugaji ni
maeneo makame ambayo hayana miti ya kutosha kutokana na miti hiyo kuliwa
na mifugo hali inayosababisha kuwepo na changamoto ya upepo mkali
unaoezua nyumba za wananchi hao .
"ukiangalia hata nyumba nyingi zinazoezuliwa paa katika maeneo mbalimbali utagundua ni kwa sababu hakuna miti,"Alisema
Kwa
upande wa wananchi hao Meishili Kivuyo anasema wao kama wajumbe wa
serikali ya mtaa wanaahidi kuwa watunzaji wazuri wa miti hiyo kwa kuwa
changamoto ya kuezuliwa nyumba ni kubwa.
Vilevile watahakikisha
wanawekeana sheria za kuhakikisha anayeachia mifugo ikala miti hiyo
anatozwa kiasi cha shilingi elfu hamsini na hivyo kuwataka wananchi
wenzake kuwa walinzi.
Naye afisa mazingira kutoka Club hiyo ya
mazingira Lions Club Evah Benson anasema uhitaji wa miti katika maeneo
ya vijiji ni mkubwa na kwamba watahakikisha wanaendelea kupanda miti na
kutunza mazingira.
Hata hivyo miti takribani laki moja
inatarajiwa kupandwa kwa nchi nzima ambapo kwa Mkoa wa Arusha miti zaidi
ya elfu mbili imeshapandwa.
Viongozi wa lions club wakiwa na baadhi viongozi wa kata ya olmot wakionyesha miti wanayokwenda kupanda katika eneo lenye ukame.
Vijana wa kata ya Olmoti wakiongoza zoezi la upandaji miti.
Meya wa Jiji la Arusha wa pili kushoto Maximilian Iraghe akitoa maelekezo kwa wadau wa mazingira.
Afisa mazingira wa Lions club akimkabidhi kaimu mganga mkuu wa jiji mti kwaajili ya kupanda mti huo.
Meya wa jiji la Arusha Maximilian Iraghe akipanda mti katika hospital ya wilaya ya Arusha
Picha ya pamoja wadau wa mazingira.
No comments:
Post a Comment