Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na
Mazingira wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,
Dkt. Andrew Komba wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua shughuli za
kilimo msitu ya alizeti katika shamba darasa lililopo Kijiji cha Haubi
Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo Machi 12, 2022,
kupitia Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa
Chakula katika Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa na Ofisi ya
Makamu wa Rais.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na
Mazingira, Mhe. David Kihenzile akisisitiza jambo wakati wa ziara ya
kamati hiyo kujionea shughuli ya utengaji wa msitu wa Intela wenye
ukubwa wa hekta 863.4 kuwa hifadhi ya kijiji cha Haubi wilayani Kondoa
mkoani Dodoma chini ya Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na
Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na
kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ziara iliyofanyika leo Machi 12,
2022.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis
Hamza Khamis akifafanua jambo kuhusu taarifa ya Mradi wa Kurejesha Ardhi
iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo Kame
Tanzania (LDFS) ambao unaratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais mbele ya
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira
leo Machi 12, 2022 wilayani Kondoa mkoani Dodoma.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na
Mazingira wakiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua shughuli ya
utengaji wa msitu wa Intela wenye ukubwa wa hekta 863.4 kuwa hifadhi ya
kijiji cha Haubi wilayani Kondoa mkoani Dodoma chini ya Mradi wa
Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika
Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais,
ziara iliyofanyika leo Machi 12, 2022.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na
Mazingira wakiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua Mradi wa
Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika
Maeneo Kame Tanzania (LDFS) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais
katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo Machi 12, 2022.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Sunday, March 13, 2022
KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA MRADI WA MAZINGIRA KONDOA, DODOMA
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment