Waziri
wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu [Kazi Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu]
Prof.Joyce Ndalichako amewaelekeza viongozi wa vyama vya wafanyakazi
waweze kumaliza makosa ya yasio ya jinai kwa watumishi wa umma katika
sehemu zao za kazi
Prof.Ndalichako ameyasema hayo Machi 12,2022
katika ukumbi uliopo Rayal hotel jijini Dodoma wakati akifungua mkutano
wa baraza kuu la shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania
[TUCTA] ambapo amesema haipaswi kuwekwa ndani watumishi wa umma kwa
makosa yasiyo ya jinai kwani pamekuwa na tabia ya wakuu wa wilaya na
wakuu wa mikoa kuwaweka ndani watumishi wa umma kwa makosa yasio ya
jinai.
Hivyo,amesema makossa ya kiutendaji kwa watumishi yachukuliwe hatua sehemu za kazi.
Aidha,Prof.Ndalichako
amewaagiza waajiri wote nchini kuhakikisha vikao vya mabaraza ya
wafanyakazi vifanyike kwa mujibu wa matakwa ya kisheria ikiwemo kulipa
posho stahiki kwa wafanyakazi Kwa upande wake rais wa shirikisho la
vyama vya wafanyakazi Tanzania [TUCTA] Tumaini Nyamhokya amesema kuna
haja kwa serikali kutekeleza ipasavyo kuwarejesha kazini watumishi wa
darasa la saba kwani kuna baadhi ya taasisi zimekuwa zikiwakataa na
kuwanyima stahiki zao huku mwenyekiti wa kamati ya wanawake wa
shirikisho hilo Rehema Ludanga akibainisha kuwa bado kuna changamoto ya
utekelezaji wa sheria ya mkataba wa kazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na viongozi pamoja na wajumbe wa baraza kuu la shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania [TUCTA] wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) uliofanyika katika ukumbi wa Royal Hotel jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment