LEO
dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1688.99 na kuuzwa kwa
shilingi 1679.55 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi
50.0613 na kuuzwa kwa shilingi 50.5044.
Hayo
ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za
kigeni iliyotolewa leo Machi 21, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha,
Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 152.7 na kuuzwa kwa
shilingi 154.2 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.01 na
kuuzwa kwa shilingi 20.2.
Franka
ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21
huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2287.0 na kuuzwa
kwa Shilingi 2309.9.
Aidha,kwa
mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3004.7 huku
ikiuzwa kwa Shilingi 3035.7 na Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi
2523.302 na kuuzwa kwa shilingi 2549.46.
Yuan
ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.6 huku ikiuzwa kwa shilingi
363.14 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.21 na kuuzwa kwa
shilingi 19.39.
Wakati
huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.21 na kuuzwa kwa
shilingi 2.28 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na
kuuzwa kwa shilingi 0.64.
Kwa
mujibu wa Benki Kuu, Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)
inanunuliwa kwa shilingi 622.7 na kuuzwa kwa shilingi 628.81 huku sarafu
ya Austria ya Schilling (ATS) ikununuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa
kwa shilingi 148.1.
No comments:
Post a Comment