SERIKALI
ya Korea kupitia taasisi yake ya Korea Foundation for International
Healthcare (KOFIH) imetoa kiasi cha Sh.milioni 232 kwa ajili ya
kufadhili ukarabati wa chumba cha kutakasia vifaa tiba katika Hospitali
ya Rufaa ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani.
Ukarabati
wa chumba hicho ulianza mapema mwaka huu na tayari kimekamilika wiki
iliyopita ambapo Balozi wa Korea hapa nchini, Kim Sun Pyo alikuwa mgeni
rasmi katika makabidhiano na uzinduzi wake.
Akiwa
katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika juzi hospitalini hapo Balozi
Pyo amesema kuwa, Serikali ya Korea inatambua changamoto zilizopo katika
Sekta ya Afya hapa nchini ndio maana wanajitoa katika kusaidia.
Pyo
amesema kuwa, msaada huo sio wa kwanza bali Serikali ya Korea kupitia
taasisi yake ya KOFIH ilianza kusaidia Hospitali ya Tumbi katika
kukarabati wodi ya watoto mahututi (ICU ya watoto) chini ya siku 28
(Neonatal Intensive Care Unit).
Aidha,amesema
kutokana na umuhimu wa sekta ya afya nchini Serikali ya Korea
itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha wanaendelea
kutatua changamoto zote zilizopo katika sekta afya.
"Msaada
huu tuliotoa hapa hospitali ya Rufaa ya Tumbi utakuwa endelevu, lakini
tutafika katika hospitali nyingine zilizopo hapa nchini kwa kuwa lengo
letu ni kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutatua changamoto za
afya,"amesema Pyo.
Pyo
ameongeza kuwa, uchumi imara wa nchini unajengwa na wananchi wenye afya
njema ndio maana taasisi yake imejikita katika masuala ya afya na
kwamba anaamini kupitia ushirikiano huo Tanzania itakuwa na watu imara
katika kujenga uchumi.
Awali
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi,Dkt.Amaani
Malima, ameishukuru Serikali ya Korea kupitia Taasisi ya KOFIH kwa
ufadhili mkubwa waliohufanya hospitalini hapo.
Dkt
.Malima amesema kuwa, kutokana na ongezeko la uhitaji wa vifaa tiba
safi na salama vilivyotakaswa kwa kufuata sheria na taratibu za kitabibu
na kukidhi mahitaji ya wagonjwa uongozi wa Hospitali uliona kuna
umuhimu wa kuwa na chumba cha kutakasia vifaa tiba.
Amesema,
upatikanaji wa chumba hicho utasaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa
wagonjwa ambao ni majeruhi,wahitaji wa huduma za upasuaji,huduma za
kusafisha vidonda na huduma nyingine zinazohusiana.
"Natumia
fursa hii kuishukuru Serikali ya Korea kupitia Taasisi ya KOFIH kwa
msaada huo muhimu ambao umekuja wakati muafaka,chumba hiki cha kutakasia
vifaa tiba kitarahisisha upatikanaji wa utakasaji wa vifaa kwa wagonjwa
ili kupunguza maambukizi,"amesema Dkt.Malima.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dkt.Gunini Kamba,amesema kuwa katika fedha hizo
vifaa na ukarabati wa vyumba vya kutakasia imetumika Sh. milioni 52.6
huku ununuzi wa mashine na kusimika ni Sh. milioni 179.9.
Dkt.Kamba,
amesema chumba cha kutakasia vifaa tiba kimegawanyika katika vyumba
vinne kikiwemo chumba cha kupokelea vifaa vilivyotakaswa kwa wagonjwa na
kuvisafisha,chumba cha kuchemshia vifaa,chumba cha kuandalia vifaa
tayari kwenda kuchemshwa na chumba cha kuhifadhia na kutolea vifaa
vilivyosafi na salama.
Hata
hivyo,Dkt.Kamba ameiomba Taasisi ya KOFIH kuendelea kusaidia hospitali
hiyo katika ujenzi wa wodi ya mama na watoto ili kurahisisha utoaji wa
huduma pindi wanapokuja hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment