A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, March 18, 2022

Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Machi 18,2021

 

LEO Krona ya Uswidi (DKK) inanunuliwa kwa shilingi 339.6 na kuuzwa kwa shilingi 342.905 huku dola ya Marekani nchini inanunuliwa kwa Shilingi 2287.04 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.91.
Kwa upande wa Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) inanunuliwa kwa shilingi 622.73 na kuuzwa kwa shilingi 628.80 huku Dola ya Australia (AUD) ikinululiwa kwa shilingi 1658.3252 na kuuzwa kwa shilingi 1678.23.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Machi 18,2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Aidha, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3001.74 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3032.912 huku Euro ya Ulaya ikinunuliwa kwa shilingi 2526.95 na kuuzwa kwa shilingi 2553.14.

Wakati huo huo Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 360.46 na kuuzwa kwa shilingi 363.6 huku Randi ya Afrika Kusini ikinunuliwa kwa shilingi 152.962 na kuuzwa kwa shilingi 154.442.
Kwa upande wa shilingi ya Kenya inanunuliwa kwa ashilingi 20.0 na kuuzwa kwa shilingi 20.1 huku Franka ya Rwanda ikinunuliwa kwa shilingi 2.23 na kuuzwa kwa shilingi 2.29.

Shilingi ya Uganda inanunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64 huku Franka ya Burundi ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages