A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 21, 2022

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 21.03.2022: Haaland, Phillips, Tchouameni, Barella, Dybala, Koeman

_123780088_dd547fb6-9f68-48bd-86b0-839cd3c52029

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Manchester City hawaamini kwamba wana nafasi kubwa ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland na Real Madrid wanaweza kujaribu kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kusalia Borussia Dortmund kwa msimu mmoja zaidi kabla ya kujaribu kumsajili. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Kiungo wa kati wa zamani wa Real Madrid Guti anasema klabu hiyo haitaweza kumsajili Haaland iwapo itashindwa kumnasa msimu huu wa joto. (El Chiringuito, via Goal)

_123780090_751f9654-5b25-4fb7-881e-f05b4ecef8ce

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelotti anataka kumsajili kiungo wa kati wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 25 Nicolo Barella na kuwasili kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia kunaweza kuweka shaka juu ya mustakabali wa Mjerumani Toni Kroos, 32, katika klabu hiyo ya Bernabeu. (El Nacional - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Aurelien Tchouameni anavutia Chelsea, Liverpool, Paris St-Germain na Real Madrid lakini Monaco hawatakubali chini ya euro 50m (£42m) kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Foot Mercato - in French)Aston Villa wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Leeds United Kalvin Phillips, 26, na wako tayari kulipa pauni milioni 60 kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Times - subscription required)

_123780092_c0c40f34-2b3b-4722-8f82-0e780bf40ad5

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri anasema hajui kama fowadi wa Argentina Paulo Dybala atakuwa katika klabu hiyo msimu ujao, huku kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ikimalizika msimu wa joto. (DAZN, via Football Italia)

Beki wa kushoto wa Brazil Marcal, 33, anakaribia kuondoka Wolves mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto na kusaini mkataba wa kujiunga na Botafogo ya nchini kwao. (Globo Esporte)

_123780197_bd7c0577-dfa5-4a07-87ae-02bc36da527a

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kocha wa zamani wa Barcelona Ronald Koeman yuko kwenye mazungumzo kuhusu kurejea katika nafasi yake ya meneja wa timu ya taifa ya Uholanzi na kurithi mikoba ya kocha wa sasa wa Uholanzi Louis van Gaal, ambaye mkataba wake unamalizika baada ya Kombe la Dunia la 2022. (NOS - in Dutch)

Roma na Hellas Verona wanavutiwa na mchezaji wa Chelsea Charly Musonda, 25, huku Mbelgiji huyo akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Stamford Bridge msimu wa joto. (Goal)

Manchester United inamfuatilia mlinda mlango wa Uswizi Benjamin Siegrist, 30, ambaye anachezea Dundee United na mkataba wake unamalizika msimu wa joto. (Mirror)

_123780095_mediaitem123780093

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Beki wa kulia wa Chelsea Reece James, 22, anatazamiwa kujiondoa kwenye kikosi cha Uingereza na beki wa Crystal Palace Tyrick Mitchell, 22, ataitwa kuchukua nafasi yake. (Mail)

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages