Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah,
akihutubia kwenye hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais
Samia Suluhu Hassan iliyofanyika makao makuu ya chama hicho mkoani hapa
jana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Mwiru akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu akizungumza kwenye hafla hiyo
wakati akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya
maendeleo.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Viongozi wa CCM na Wazee wakiwa kwenye hafla hiyo.
Makofi yakipigwa kwenye hafla hiyo.
Viongozi
wakiwa meza kuu. Kutoka kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Lucy
Boniphace, Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Singida Alhajj Juma
Killimbah, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Mwiru na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wakuu wa Idara za Serikali na Wataalamu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wakuu wa Idara za Serikali na Wataalamu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida Vaileth Soka akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga akizungumza wakati
akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida DC, Eliya Digha akizungumza wakati
akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi akizungumza wakati
akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi , Hussein Simba akizungumza wakati
akitoa taarifa ya fedha walizozipokea kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wenyeviti
wa Halmashauri za wilaya wakiwa kwenye hafla hiyo. kutoka kushoto ni
Ally Mwanga (Ikungi), Innocent Msengi (Iramba) na Eliya Digha Singida
DC.
Viongozi
wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya
Ikungi Stamili Dendegu, Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa
Singida, Asha Stambuli na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa
wa Singida, Vaileth Soka.
Taswira ya hafla hiyo.
Furaha tupu katika hafla hiyo
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Makatibu wa CCM wa Wilaya wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Mwenge wakiwa kwenye hafla hiyo ya kumpongeza
Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi wake.
Hafla ikiendelea.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Singida Alhajj Juma Killimbah
amesema fedha za kutekeleza miradi zilizoletwa mkoani hapa na Rais Samia
Suluhu Hassan kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika
kipindi cha mwaka 2021/2022 kuanzia Julai 2021 hadi Februari 2022 ziwe
chachu ya maendeleo kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.
Killimbah
aliyasema hayo katika hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wa
Rais Samia Suluhu Hassan iliyofanyika makao makuu ya chama hicho mkoani
hapa jana.
“Fedha hizi zilizotetwa na Mama yetu katika mkoa wetu
ziwe chachu ya maendeleo kwa mwaka huu unaokuja” alisema Killimbah huku
akishangiliwa na mamia ya Wananchi na Wana CCM waliohudhuria hafla
hiyo.
Alisema miradi inayokuja mahala popote fedha hizo
zinatafutwa na Rais wetu kwa juhudi kubwa na wabunge wanasimamia bajeti
ili ije Singida kwa ajili ya kuleta maendeleo.
Killimbah
alitumia mkutano huo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo
makubwa ya maendeleo aliyoufanyia Mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Boniphace akizungumza kwenye hafla hiyo
alisema kwa mwaka mmoja alioongoza Rais Samia Suluhu Hassan Mkoa wa
Singida umepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwani wilaya zote wamepokea
fedha nyingi za maendeleo.
Alisema sambamba na hilo Rais Samia
Suluhu Hassan amekuwa akikutana na makundi mbalimbali kwa lengo la
kuwasikiliza na kupokea maoni yao kwa ajili ya kujenga nchi yetu na
kuwa huo ni ukomavu mkubwa wa kisiasa na kujiamini katika utendaji wake
wa kuongoza nchi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Singida DC, Eliya Digha akizungumza wakati akitoa taarifa ya maendeleo
ya wilaya hiyo alimfananisha Rais Samia Suluhu Hassan na mwanamke mmoja
shujaa aliyetajwa kwenye Biblia aitwaye Esther ambaye alijulikana sana
kwenye Taifa la Waisrael.
“Rais wetu Mama Samia amefanya mambo mema na makubwa katika nchi hii hivyo tunakila sababu ya kumpongeza” alisema Digha.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Mkoa wa Singida Yohana Msita alisema
Rais Samia Suluhu Hassan hakika ameupiga mwingi hapa nchini kwa kazi
kubwa aliyoifanya ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani.
Alisema
Rais Samia hakuna sehemu aliyoiacha bila ya kuifikia kwa maendelea
katika sekta zote na ameonesha uwezo mkubwa wa kuongoza nchi ambapo
aliwaomba watanzania kuendelea kumuombea kwa Mungu na kuunga mkono
jitihada zakezote za maendeleo anazozifanya.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Singida Mjini Lusia Mwiru alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan
kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo
alitumia nafasi hiyo kuwaomba Wana CCM wenye sifa ya kugombea nafasi
mbalimbali kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea katika uchaguzi wa ndani
utaofanyika hivi karibuni.
Katika hafla hiyohiyo kila wilaya
mkoani hapa ilitoa taarifa ya fedha walizopokea kwa ajili ya utekelezaji
wa miradi ya maendeleo walioifanya ambayo ziliwasilishwa na Wenyeviti
wa Halmashauri husika ambapo katika Wlaya ya Ikungi Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Ally Mwanga alisema walipokea Sh.11,263,030,397 ambazo
zilitumika katika Elimu, Afya, Utawala, Mfuko wa Jimbo, Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira
(RUWASA), Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Mamlaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Singida (SUWASA).
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi alisema wao
walipokea Sh.10,960,988,976 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo huku
Wilaya ya Itigi wakipokea Sh.7,435,318,522 na Manyoni
Sh.10,505,419,366.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
walipokea Sh.7,811,623,781, Singida DC Sh.10,046,768,035, Singida
Manispaa Sh.5,791,791,192, Sekretarieti ya Mkoa Sh.875,552,414, Tanesco
Sh.63,507,622,522, Jumla Kuu ikiwa ni Sh.128,198,115,205.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, March 21, 2022
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment