MKUU
wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa katikati akisisitiza jambo wakati
wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Tanga ambao hawapo pichani
kuhusu Tamasha la Utamaduni ( Tanga Utalii Festival) linalotarajiwa
kufanyika Jumamosi wiki hii Jijini Tanga kulia ni Meneja wa Bia ya
Heineken Kanda ya Kaskazini, Swalehe Madjapa ambao ni mdhamini mkuu wa
tamasha hilo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga
MKUU
wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa katikati akisisitiza jambo wakati
wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani Tanga ambao hawapo pichani
kuhusu Tamasha la Utamaduni ( Tanga Utalii Festival) linalotarajiwa
kufanyika Jumamosi wiki hii Jijini Tanga kulia ni Meneja wa Bia ya
Heineken Kanda ya Kaskazini, Swalehe Madjapa ambao ni mdhamini mkuu wa
tamasha hilo kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga
Meneja
wa Bia ya Heineken Kanda ya Kaskazini, Swalehe Madjapa ambao ni
mdhamini mkuu wa tamasha hilo akizungumza wakati wa mkutano huo kushoto
ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua matukio kwenye mkutano huo.
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
TAMASHA
la Utamaduni ( Tanga Utalii Festival) linalotarajiwa kufanyika Jumamosi
wiki hii Jijini Tanga litatumika pia kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu
na Makazi linayotarajiwa kufanyika nchini Agosti mwaka huu ikiwemo
kutangaza fursa za utalii, uchumi na utamaduni katika tamasha hilo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa katika
mkutano wake na vyombo vya habari uliofanyika wilayani hapa kuhusu
kuelekea Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuwa na aina yake
Mgandilwa amesema wamekusudia kufanya tamasha hilo kutangaza fursa
mbalimbali zinazopatikana mkoani humo pamoja na kutangaza tamaduni
mbalimbali za makabila yanayopatikana Tanga.
"Watanzania moja
ya jambo tunalojivunia na tunapaswa kuenzi ni tamaduni zetu, sisi
katika ngazi ya wilaya tumeliona hilo na tumeazimia kufanya tamasha
liyakalohusisha tamasuni za watu wa Tanga, hivyo tutakuwa na ngoma
mbalimbali," amesema.
Mgandilwa amezitaja ngoma za asili
zitakazoshiriki katika tamasha hilo kuwa ni mdumange, baikoko, singeli
pamoja na msanja pia kutakuwa na wasanii maarufu wa muziki wa kizazi
kipya akiwamo Matonya, Kassim Mganga na Dula makabila.
Kwa
upande wake Meneja wa Bia ya Heineken Kanda ya Kaskazini, Swalehe
Madjapa ambao ni mdhamini mkuu wa tamasha hilo, amesema wameamua
kudhamini tamasha hilo kutokana na umuhimu wake kwa watu wa Tanga.
"Bia
ya Heineken tumeona umuhimu wa tamasha hilo katika katika kuutangza
Mkoa wa Tanga kimataifa tunaamini kuna fursa nyingi za kiuchumi hivyo
tunaamini kupitia tamasha hili tutawavutia wawekezaji," Amesema
Swalaehe.
Naye Mratibu wa tamasha hilo,Nasoro Makau ameviasa
vyombo vya habari nchini kuzitangaza nyimbo za asili ili kuendelea
kuuenzi utamaduni wa mtanzania.
"Vyombo vya habari vinatangaza
sana muziki wa kizazi kipya sasa vione umuhimu pia wa kutangaza
utamaduni wetu watoto wetu nao watambue kuwa tuna nyimbo zetu za asili
wasije wakabobea kwenye tamadunii za kimagharibi na kuacha tamaduni zao.
"Tamasha litakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo mbio fupi,
burudani kutoka kwa wasanii tofauti kwa hiyo kwa wenyeji wa Tanga
tunawasihi kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Jengo la Urithi,
tamasha litaanza saa 12 asubuhi na halina kiingilio. Kauli mbiu ya
tamasha hilo ni 'Tanga Festival, karibu mahabani," amesema
Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, March 23, 2022
TANGA UTALII FESTIVAL KUHAMASISHA ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment