Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
akikata utepe kuzindua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali
kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota
Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
akiondoa kitambaa kuzindua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali
kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota
Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
akikabidhi mfano wa Ufunguo kwa Bibi Mwajuma Sama na Mzee Henry Ngwemba
kwa ajili ya kuwakabidhi Nyumba mara baada ya kuzindua rasmi mradi wa
Nyumba 644 Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi 2022. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
akikagua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa
Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam
leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Dar Es salaam baada ya kuzindua mradi
wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo
Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam leo
tarehe 23 Machi, 2022.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Msanifu
majengo Daud Kondoro wakati alipokuwa akitoa maelezo kuhusu hatua
mbalimbali za Ujenzi wa Nyumba 644 katika eneo la Magomeni Kota Mkoani
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
akiagana na Viongozi wa Mkoa wa Dar Es salaam na Wakala wa Majengo
Tanzania TBA baada ya kuzungumza na Wananchi na kuzindua mradi wa Nyumba
644 zilizojengwa na Serikali kupitia TBA katika eneo la Magomeni Kota
Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa
maelekezo kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuruhusu wananchi wa Magomeni
Kota kuuziwa nyumba kwa utaratibu wa mpangaji ununuzi.
Rais
Samia ametoa maelekezo hayo leo wakati akizindua nyumba 644 za makazi
za Magomeni Kota Jijini Dar es Salaam ambazo ujenzi wake umegharimu
zaidi ya shilingi Bilioni 52.
Wakazi
hao ambao wameahidiwa kukaa bure kwa miaka mitano, wameruhusiwa kulipa
gharama za ujenzi wa nyumba pekee bila ya gharama za ardhi na
miundombinu ya jumuiya baada ya miaka hiyo.
Hata
hivyo, wakazi wanaotaka kulipa gharama ya ununuzi kabla ya kufika miaka
mitano wanaruhusiwa kulipa kidogo kidogo kwa kipindi cha miaka 10 bila
ya riba yoyote.
Rais
Samia amewasihi wakazi hao kutunza nyumba hizo na kuzingatia usafi wa
ndani na nje na kuchangia huduma jumuishi kwa faida ya kila mmoja.
Aidha,
Rais Samia amewataka TBA, NHC na Watumishi Housing kukaa na sekta
binafsi ili kukubaliana katika ujenzi wa makazi bora kwenye maeneo
yanayopaswa kuendelezwa.
Mahitaji
ya nyumba bora yanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 3 nchi nzima, huku
ongezeko la mahitaji ya nyumba bora ni takribani laki mbili kila mwaka.
Wakati
huo huo, Mhe. Rais Samia amefanya mazungumzo ya kushirikiana katika
maendeleo mbalimbali hasa kwenye masuala ya miundombinu na nishati na
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Africa50, Alain Ebobisse aliyeambatana na
Ujumbe wake Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
ZuhuraYunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
No comments:
Post a Comment