SERIKALI
imewataka viongozi wa dini nchini kuwaelimisha waumini wake umuhimu wa
kuhesabiwa katka Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi
Agosti, mwaka huu.
Askofu
wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Flavian Kassala akikata utepe wa
ufunguzi wa Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima. Wa pili kulia ni
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula
ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Askofu
wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Flavian Kassala akifungua rasmi
lango Kuu la Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita katika hafla
ya Kutabaruku kanisa hilo iliyofanyika Machi 20,2022.
Aidha,
imewataka viongozi wa dini kuendelea kusaidia katika suala zima la
malezi ya kiroho ili kujenga jamii yenye kumcha Mungu, uadilifu na
ubinadamu.
Akizungumza
kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa Kutabaruku Kanisa
la Bikira Maria wa Fatima Geita tarehe 20,2022, Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula amesema, Tanzania imebarikiwa
kuwa na rasilimali nyingi ambazo bila ya kuwa na takwimu sahihi
haitaweza kupanga mipango thabiti ya matumizi endelevu ya rasilimali
hizo.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akimpatia
zawadi Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhashamu Flavian Kassala
wakati wa hafla ya kutabaruku Kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima
Geita.
‘’Viongozi
wa dini mnao waumini wengi tumieni fursa hiyo kuwaelimisha waumini wenu
umuhimu wa kuhesabiwa,’’ ilieleza hotuba ya Waziri Mkuu.
Alisema,
zoezi la sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa kuwa linaipatia nchi
takwimu za msingi zinazotumika kutunga sera, kupanga mipango na program
za maendeleo pamoja na kufuatilia utekelezaji wake.
Kupitia
hotuba hiyo, Dkt.Mabula alieleza kuwa, takwimu rasmi zitawezesha
serikali na wadau wengine kufuatilia na kutathmini malengo yaliyofikiwa
katika kutekeleza mipango ya maendeleo iliyokusudiwa sambamba na
changamoto mbalimbali zitakazojitokeza katika sekta zote na hatimaye
kuweka malengo na mikakati ya kukuza uchumi pamoja na kupunguza
umasikini miongoni mwa watanzania.
Askofu
wa Jimbo Katoliki la Geita Mhasham Flavian Kassala akipaka moja ya
nguzo 12 za Kanisa mafuta ya krisma ndani ya kanisa mbele ya waumini
wakati wa hafla ya kutabaruku Knisa jipya la Bikira Maria wa Fatima
Geita.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikabidhi
cheti kwa baadhi waumini wakati wa hafla ya kutabaruku Kanisa jipya la
Bikira Maria wa Fatima Geita.
Aidha,
ilieleza kuwa, hivi karibuni kumekuwa matukio yanayohusisha mauaji ya
raia kwa raia , moto kwenye masoko na baadhi ya raia kujinyonga ambapo
alisema tayari serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo
kulitaka jeshi la polisi kuweka mikakati ya kuhakikisha jamii inatoa
taarifa sahihi zitakazosaidia kukabiliana na vitendo vya kihalifu.
‘’Niwaombe
viongozi wetu wa taasisi za dini kuendelea kusaidia katika suala zima
la malezi ya kiroho ili kujenga jamii yenye kumcha Mungu, uadilifu na
ubinadamu," ilieleza hotuba ya Waziri Mkuu.
Kwa
upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Geita, Mhashamu Baba Askofu
Flavian Kasala ambaye ni Padre wa kwanza wa Parokia hiyo ya Bikira Maria
wa Fatima tangu kuanzishwa kwake alisema, viongozi wa dni wataendelea
kuiunga mkono serikali katika suala zima la sensa ya watu na makazi kwa
kuwa suala hilo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya waumini waliochangia Samani za Kanisa
jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita kwenye hafla maalum ya Kutabaruku
kanisa hilo ambapo alimuwakilisha Waziri Mkuu.
‘’Sisi
tutaendelea kuinga mkono serikali na uwepo tofauti ndogo ndogo ndizo
zimewapeleka baadhi ya watu kwenye matatizo makubwa na tusiruhusu jambo
hilo linaloweza kututofautisha kwenye imani zetu za kidini,’’alisema
Askofu Flavian Kasala.
Hafla
ya kubariki Kanisa la Bikira Maria wa Fatima Jimbo la Geita ambalo
ujenzi wake ulianza Januari 3, 2020 na kukamilika Machi 18, 2022 na
kugharimu takribani shilingi Bilioni 1.9 iligawanyika sehemu ya
kutabaruku kanisa kwa kunyunyizia maji ya Baraka nje na ndani ya kanisa,
kupaka mafuta ya krisma altare mpya pamoja na nguzo 12 na kuendelea na
ibada ya misa takatifu iliyoanza saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula
akiwahutubia waumini waliohudhuria hafla ya Kutabaruku Kanisa la Bikira
Maria wa Fatima Geita iliyofanyika Machi 20,2022 ambapo alimuwakilisha
Waziri Mkuu.
Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akiwa
katikati ya Mapadre wakati wa kuendesha harambee ya kuchangia samani za
kanisa jipya la Bikira Maria wa Fatima Geita katika hafla maalum ya
Kutabaruku kanisa hilo ambapo alimuwakilisha Waziri Mkuu.
Aidha,
kupitia hafla hiyo Dkt.Angeline Mabula aliongoza harambee kwa ajili ya
kuchangia ukamilishaji samani za kanisa ambapo kiasi cha shilingi
88,725,000 kilipatikana kwa fedha taslimu na ahadi kutoka kwa watu
mbalimbali.
‘’Uwepo
wa jengo hili jipya, kubwa na zuri la Kanisa la Bikira Maria wa Fatima
ni ushuhuda wa kukua kwa imani ya kanisa kwa waumini wake ambapo sasa ni
miaka 65 imepita tangu injili ilipoingia ukanda huu wa Altare ya kwanza
ya Jimbo la Geita ilikuwa katika uwanja lililopojengwa jengo hili
jipya,’’ alisema Askofu Kasala.
No comments:
Post a Comment