Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa wa Mapambano
dhidi ya UVIKO -19 imetenga shilingi bilioni 1.01 kwa ajili ya mafunzo
ya kuwajengea uwezo waongoza watalii wanawake takribani 1060 nchini.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja
(Mb) wakati wa kuhitimisha mafunzo ya waongoza Watalii wanawake 89
yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
“Mafunzo haya
ni mahususi kwa wanawake kama jitihada za makusudi kabisa za Serikali
kuhakikisha kuwa wanawake wanapata fursa za kuchangia katika maendeleo
ya nchi kupitia utalii na kunufaika kupitia sekta hiyo” ” amefafanua
Mhe. Masanja.
Amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri kwa kuitangaza vyema Tanzania ndani na nje ya nchi.
“Natambua mmekuwa mabalozi muhimu mnaotegemewa kuiuza nchi yetu hivyo
sifa ya kwanza mnayotakiwa kuwa nayo ni uzalendo. Wageni mnaowapokea
wana sifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa hivyo wakati mnatekeleza
majukumu yenu mnapaswa kuwa na uelewa mpana wa shughuli za utalii na pia
muwe na maadili, weledi na uadilifu”amesema Mhe. Masanja.
Aidha,
amewaasa waongoza watalii hao kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa
watalii wanapowasili nchini ili kujenga taswira nzuri ya Tanzania na
kumfanya mtalii aweze kurudi.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza
wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waongoza watalii
wanawake yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mkuu
wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA), Prof. Jafari Kideghesho
akitoa neno la utangulizi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea
uwezo waongoza watalii wanawake yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Maliasili na
Utalii,Dkt. Consolatha Kapinga akielezea namna Serikali ilivyojipanga
kuwawezesha wanawake hasa kuwajengea uwezo waongoza watalii, wakati wa
kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waongoza watalii wanawake
yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsilikiza
Kiongozi Mkuu wa Waongoza Watalii Wanawake Tanzania,Maggie Dankan
Simbeye (kulia) akifafanua kuhusu hema linalotumika kiutualii
alipowasili kuhitimisha mafunzo ya kuwajengea uwezo waongoza watalii
wanawake yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya waongoza watalii wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)(hayupo pichani)
wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, March 19, 2022
SERIKALI YATENGA BILIONI 1 KWA AJILI YA MAFUNZO YA WAONGOZA WATALII WANAWAKE NCHINI
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment