Mkuu wa Kitengo cha Biashara-GetPaid, Bw. Justine Mahinyila, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa la GetPaid, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Mpiga Picha Wetu
Washiriki wakifuatia mijadala jinsi ya kutumia la Jukwaa la GetPaid, wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa hili jijini Dar es Salaam jana. (Mpiga Picha Wetu)
Jukwaa la “GeitPaid” kutoa fursa kwa watanzania
Na Mwandishi Wetu
Jukwaa la Kijidital, “GetPaid” lenye lengo la kutoa fursa za Ajira na nyinginezo limezinduliwa jana jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mchango wa sekta binafsi kusaidia mikakati ya serikali inayolenga kupanua wigo wa fursa kwa vijana na watanzania kwa ujumla.
Mbali na mambo megine Jukwaa la GetPaid, litasaidia Tanzania kupunguza wimbi kubwa la ukosefu wa ajira—kwa vijana na watanzania wote (wasomi na wasio soma, amesema Bw. Richard Lema, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania DLT CP iliyobuni na kutengeneza Mtandao wa GetPaid—wakati wa uzinduzi rasmi wa Jukwaa hilo jijini Dar es Salaam jana.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Lema, GetPaid ni jukwaa la kimkakati la kidijitali ambalo lengo lake kuu ni kuwaunganisha watanzania, ikiwa nia pamoja na vijana, wafanyabiashara, wasomi, wasio soma, wajasiriamali, wanaofanyakazi binafsi na fursa mbalimbali duniani.
"Kwa kweli, hili ni jukwaa la kidijitali la pekee, ambalo linawaunganisha watu—wasaka fursa na watoa fursa, " ameongeza Bw. Lema
Alielezea GetPaid kama ni teknolojia ya kisasa, ambayo itawaunganisha watu na fursa mbalimbali kitaifa, kikanda na kidunia.
Kwa njia ya jukwaa la GetPaid, watu wa aina mbalimbali – wazalishaji, wafanyabiashara, wanaofanya kazi binafsi, watu wazima, vijana, wenye weledi na wasio na weledi - watawezeshwa kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo Afrika na nje ya Afrika.
"Jukwaa la GetPaid linawafanya waweze kunufaika na fursa mbalimbali duniani, elimu ya kidijitali na uvumbuzi. Hili linafanyika kupitia kikundi cha jumuiya, utumiaji rahisi na elimu," alisema Bw. Lema na kuongeza kwamba "bidhaa ya GetPaid ina vitu vitatu na inawapa watumiaji (waanzilishi, wafanyabiashara na wafanyakazi binafsi vifaa na elimu wanayohitaji kuishi, kufanyakazi na kupata ujira."
Akizungumza wakati wa uzinduzi, mtaalamu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari (ICT) Baraka Mafore alisema ingawa kuna ukuaji wa kasi wa uchumi wa kidijitali, bado kuna pengo kubwa linalotakiwa lijazwe, kwa vile mamilioni ya vijana katika nchi nyingi za Afrika hawana ajira.
Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba pamoja na kwamba vijana wanaomaliza chuo na kuingia kwenye soko la kazi Tanzania wanaanzia 800,000 hadi 1,000,000 kila mwaka (NBS-2015), kwa wastani uchumi unatengeneza ajira zipatazo 250,000 tu kwa mwaka na asilimia 75 ya hawa vijana wanabaki bila ajira.
"Hata hivyo, kutumia njia na vifaa sahihi, kama jukwaa la GetPid, nchi za Afrika zinaweza kushuhudia idadi kubwa ya vijana wakijiunga na kuingia kwenye uchumi wa kidijitali," alisema mhitimu mmoja kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Asha Mkwezu wakati wa uzinduzi wa GetPaid APP.
DLT CP-Tanzania ni kampuni iliyosajiliwa na inamilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania wenye vipaji ambao wameingia kwenye "huu uchumi wa kidijitali."
No comments:
Post a Comment