JAJI Mkuu wa Tanzania, Prof
Ibrahim Juma ameeleza kuwa aliyekua Rais wa awamu ya tano, Dk John
Magufuli alimuagiza aliyekua Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin
Kunambi kuwapatia Mahakama kiwanja ili waweze kujenga Ofisi za Makao
Makuu ya mhimili huo.
Prof Ibrahim ameyasema hayo jana wilayani
Chato Mkoani Geita wakati wa kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha Hayati
Dk Magufuli ambacho kilitokea Machi 17 mwaka 2021.
Akizungumza
na viongozi na wananchi waliojitokeza katika Misa hiyo, Jaji Mkuu
amesema Hayati Dk Magufuli alimuita ofisini kwake kumuuliza Mpango wa
Mahakama kuhamia jijini Dodoma na ndipo alipomtaka Mkurugenzi wa Jiji
Kunambi kuwezesha upatikanaji wa kiwanja kwa ajili ya kujenga Ofisi
hizo.
" Nakumbuka Mahakama ilikua Muhimbili wa mwisho kuhamia
Dodoma, Bunge lilishatangulia halafu Serikali ikafuata, Siku moja Hayati
Dk Magufuli akaniita ofisini kwake akaniambia Nchi imehamia Dodoma nyie
Mahakama mna Mpango gani? Nikamwambia sisi tunategemea kuwezeshwa ndio
tuhame.
Ndipo akamuagiza Mkurugenzi wa Jiji ambaye Sasa hivi ni
Mbunge, Godwin Kunambi ambaye alitafuta maeneo mawili makubwa kwa ajili
ya ujenzi wetu. Tunashukuru tuliwezeshwa na leo jengo limefikia sehemu
nzuri Sana," Amesema Jaji Mkuu Prof Ibrahim.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, March 19, 2022
JAJI MKUU: MAGUFULI ALIMUAGIZA KUNAMBI ATUPATIE KIWANJA DODOMA
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment