A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 12, 2022

RC MONGELLA AZINDUA MAONESHO YA TANZFOOD JIJINI ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amezindua maonyesho ya kimataifa ya kilimo TANZFOOD EXPO huku zaidi ya makampuni 120 kutoka Tanzania na nchi jirani zikishiriki

Maonesho hayo yameandaliwa na kampuni ya KILIFAIR Promotion na kuzinduliwa jana tarehe 11/3/2022 katika viwanja vya magereza vilivyopo jijini Arusha

Baada ya kutembea mabanda mbalimbali yaliyoshiriki,Mkuu wa Mkoa Arusha John Mongella alisema maonyesho hayo ni ya siku tatu katika viwanja hivyo na lengo kubwa ni kuleta tija katika mnyororo mzima wa thamani katika kilimo,ufugaji,uvuvi pamoja na uchakataji

Mongella alisema kuwa kupitia maonyesho hayo wadau wa kilimo watapata fursa za elimu katika kujifunza na biashara huku serikali ya mkoa ikipania kufanya kimataifa

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa TAHA Dkt,Jackline Mkindi ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la kilimo Tanzania alisema kwa sasa sekta ya kilimo imefunguka na ndio inashikilia uchumi wa Taifa

"Masoko yamefunguka sana bidhaa za Tanzania zinagombaniwa kwenye masoko ya kimataifa "alisema Dkt Mkindi

Pia aliongeza kuwa Tanzania ni nchi yenye fursa ya kilimo ukizingatia imezungukwa na nchi nyingi barani Afrika ambazo zinahitaji bidhaa kutoka Tanzania

"Uwepo wa taarifa muhimu za wazalishaji ziliwezesha TAHA kushiriki katika mikutano mikubwa ya kimataifa kama Dubai,Ufaransa pamoja na ubelgiji kuangalia fursa za masoko"alisema Dkt Mkindi

Mkurugenzi wa KILIFAIR Promotion,Dominic Shoo alisema kuwa maonyesho hayo ni fursa kwa wananchi kuweza kujifunza mbinu mbalimbali za kufanya biashara pamoja na kubadilishana mawazo na fursa zilizopo

Mkuu wa Mkoa Arusha John Mongella akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua maonesho ya kimataifa ya TANZFOOD

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages