Kama
nilivyoeleza katika matini iliyotangulia namna nilivyomfahamu Mike
Mhagama ambaye alikuwa DJS wa awali na aliyewahi kuucheza muziki wa
kizazi kipya wakati huo akiwa na Redio One & ITV.
Leo hii naendelea na ndugu huyu ambaye hivi sasa yupo Marekani.
Mhagama
alisema kuwa kuwa wakati huo Joseph Haule na wenzake walikuwa
wakipatikana katika Mtaa wa Ali Khan upo Upanga Jijini Dar es Salaam na
nyuma ya mtaa huo walikuwapo jamaa zake hivyo alipokuwa akipita alikuwa
akiwakuta ndugu hawa na akizungumza nao.
“Walirekodi album yao
ya awali kabisa iliyokuwa inafahamika kama Funga Kazi, mwaka 1993
nadhani album hii haikuwa katika kiwango kinachotakiwa lakini hatimaye
mwaka 1994 walitoa album yao nyingine maarufu kama Mambo ya Mjini, album
hii ndiyo iliwatambulisha rasmi katika ulimwengu wa Hip Hop ya Tanzania
na wakawa miongoni mwa makundi yaliyokaribia kushika hatamu za muziki
huo hapo Tanzania wakati huo.”
Kulikuwa na makundi mengi ya
muziki huolakini Hard Blasterz walikuwa ni kundi tatanishi kwa makundi
mengine kama KWANZA UNITY, DIPLOMATS, DAR YOUNG MOB, WAGUMU HALISI, GANG
STARS with MATATIZO.
Nilipokuwa nikifahamiana nao kwa mara ya kwanza niligundua jambo la tofauti kabisa kwa Joseph Haule.
“Huyu
alikuwa akifahamika kama Kijana Msogo(kijana mpenda kusoma) ambaye
alikuwa akipenda shule sana sana tofauti na vijana wengine walivyokuwa
na hili lilikuwa tofauti na mitazamo ya wengi.”
Hapa Mike Mhagama alikwenda mbali zaidi ya watu wengi wanavyomfahamu Profesa Jay huku akitoa sifa ya ukimya na upole.
“Hata
katika mahojiano yaliyokuwa yakifanywa dhidi ya muziki huo, Terry
Msiaga na Wiliam Shundi wao ndiyo walikuwa wazungumzaji wakubwa huku
yeye akiwa kimya sana.”
Profesa Jay aliendelea na muziki wake na
sasa aliamua kuwa mwanamuzi binafsi. Kuanzia mwaka 2000 na jambo hilo
lilimpeleka mbali sana kisanaa na baadaye kuingia katika siasa hadi kuwa
mbunge wa Mikumi.
Profesa Jay na Sugu walionesha njia kuwa Hip
Hop haikuwa uhuni bali ilikuwa inaonesha hadharani matatizo ya jamii
ambayo yalihitaji kutatuliwa.
Mike Mhagama anamuombea heri Profesa Jay apone haraka ili aweze kuendelea na maisha yake vizuri.
Mwanakwetu
huyo ndiyo Joseph Haule kama alivyofahamiana na Mike Mhagama miongoni
mwa MadJ wa awali kabisa walioucheza muziki huo kati ya 1990- 2000 akiwa
na Redio One na ITV
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, March 12, 2022
JAY ANAYAISHI ALIYOYAIMBA IV
Tags
BURUDANI#
Share This
About kilole mzee
BURUDANI
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment