Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji
wa mkutano wa kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa mazao
ya wanyamapori na mimea ndani na nje ya Bara la Afrika.
Hayo
yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja
(Mb) wakati wa hitimisho la mkutano wa 13 wa Baraza la Uongozi la
Mkataba wa Lusaka(The 13rd Governing Council of the Lusaka Agreement)
katika kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa mazao ya
wanyamapori na mimea ndani na nje ya Bara la Afrika uliofanyika jijini
Livingston nchini Zambia.
“Nchi itafaidika na mkutano huo kwa
sababu tumekuwa na changamoto kubwa ya mapambano dhidi ya maharamia
wanaodhuru wanyama wetu na hivyo tutakomesha biashara haramu.” Mhe.
Masanja amefafanua.
Amesema mkutano huo utafanyika mwezi Mei
mwaka 2024 na unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 100 na utakuwa na
manufaa makubwa kwa Tanzania kwa sababu kuna mashirika mbalimbali ambayo
yanayojitokeza kuzisaidia nchi za Afrika ambazo zinapambana na ujangili
wa misitu na wanyamapori.
Ameongeza kuwa kama Tanzania itafikia
masharti yaliyowekwa, kitajengwa kituo cha kupambana na ujangili wa
misitu na wanyamapori jijini Arusha lengo ni kudhibiti ujangili wa
misitu na wanyamapori na kuhakikisha biashara haramu ya ujangili wa
wanyamapori na misitu inakomeshwa.
Akiongelea kuhusu Mkataba wa
Lusaka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Zambia,
Mhe.Hassan Simba Yahya amesema mkataba huo unajihusisha na kuzuia
uuzaji, usafirishaji wa wanyamapori pamoja na mimea hivyo utasaidia
katika kupambana na ujangili na uhamishaji wa wanyama na mimea ambayo
iko katika hatari za kutoweka.
Amesema Tanzania imeshiriki
katika mkutano wa 13 wa Baraza la Uongozi la Mkataba wa Lusaka katika
kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa mazao ya wanyamapori
na mimea ndani na nje ya Bara la Afrika ambao maamuzi yake yatainufaisha
Tanzania kama nchi mwanachama.
Mkutano huo umehudhuriwa na
Mawaziri Wanachama kutoka nchi za Congo, Lesotho, Liberia, Tanzania,
Uganda na Zambia. Nchi zingine zilishiriki kama Waangalizi (Observers)
ni Niger, Senegal, Angola, Malawi, Mozambique, Togo, Ivory Coast, Benin,
Ghana, Guinea , Burkina Faso na Nigeria.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, March 12, 2022
TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO KUKABILIANA NA UJANGILI BARANI AFRIKA
Tags
KIMATAIFA#
Share This
About kilole mzee
KIMATAIFA
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment