RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
anatarajia kufanya ziara Machi 22,2022 mkoani Pwani kwa ajili ya
kuzindua mradi mkubwa wa maji wa Mlandizi-Chalinze-Mboga uliogharimu
kiasi cha sh.Bilioni 18.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge ametoa taarifa hiyo leo wakati
akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika ofisi
zake zilizopo Mjini Kibaha ambapo amesema Rais atafanya ziara hiyo Machi
22,2022 ambayo ni Siku ya Jumanne.
Kunenge
amesema kuwa, Rais Samia anazindua mradi huo ikiwa ni muendelezo wa
jitihada zake za kuboresha huduma ya maji katika maeneo mbalimbali
yenye changamoto ya upatikanaji wa maji.
Amesema,mradi
huo wa bomba kuu unatarajiwa kusafirisha kiasi cha lita za ujazo
milioni tisa na laki tatu( 9,300,000) kwa siku na zitawezesha
kuwahudumia wakazi wapatao 120,912.
Amesema,
ujenzi wa mradi huo utakuwa na vituo viwili vya kusukuma maji (Boosting
Stations) vilivyojengwa katika Kijiji cha Chamakweza na Msoga ambapo
pampu sita ikiwa pampu tatu kwa kila kituo za kusukuma maji zimefungwa.
"Mheshimiwa
Rais ametupa heshima kubwa ya kuja kuzindua mradi wetu mkubwa wa maji
unaogharimu fedha nyingi kiasi cha shilingi bilioni 18 hii inaonyesha
jinsi gani anavyowapambania wananchi wa Pwani kwahiyo lazima tumpongeze
na kumshukuru kwa jitihada hizi kubwa anazofanya," amesema Kunenge.
Amesema
kuwa, Rais Samia anazindua mradi huo ikiwa ni sehemu ya kilele cha wiki
ya maji yanayofanyika Machi 22 Siku ya Jumanne huku akisema kazi
anayofanya Rais ni kubwa na anapaswa kuungwa mkono.
"Tunamshukuru
Mheshimiwa Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya Kujenga mradi
huu mkubwa wa maji ambao utasaidia kumaliza changamoto ya maji kwa
wananchi wa Mlandizi-Mboga na Chamakweza,"amesema Kunenge.
Kunenge
amesema kuwa Rais atazindua mradi huo katika eneo la Msoga na baadae
kuzungumza na wananchi katika viwanja vya Polisi vilivyopo Chalinze
ambapo amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumlaki
Rais.
"Baada
ya Rais kuzindua mradi huo katika eneo la Msoga ataelekea katika eneo
la viwanja vya Polisi Chalinze kwa ajili ya kuzungumza na wananchi
kwahiyo nawaomba wananchi wa Mkoa wa Pwani wajitokeze kwa wingi katika
mkutano huo," amesema Kunenge.
Hata
hivyo, Kunenge amewaomba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuja
kwa wingi katika kumlaki Rais kwakuwa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji
wa ilani ya chama.
No comments:
Post a Comment