NAIBU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameishukuru
Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kutenga fedha za kujenga
mipaka katika hifadhi za Taifa nchini.
Ameyasema
hayo leo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi,
Maliasili na Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mpakani mwa
Tanzania na Kenya.
Amesema,
mipaka hiyo itasaidia kupunguza migogoro kati ya hifadhi za nchi mbili
tofauti, itasaidia kudhibiti mapato yatokanayo na utalii na pia
itasaidia kudhibiti majangili.
Aidha,
ameipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuchukua
jukumu hilo kwa vitendo kujenga akitolea mfano mpaka kati ya Tanzania
na Kenya uliojengwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
No comments:
Post a Comment