RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, DkT. Hussein Ali Mwinyi ametuma salamu za pole kwa wananchi waliopatwa na maafa kufuatia upepo mkali uliotokea huko katika vijiji vya Kendwa na Nungwi Shehia ya Kiungani katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais
Dkt. Mwinyi ametoa salamu za pole kwa niaba yake, Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar pamoja na wananchi wote anatoa mkono wa pole kufuatia tukio
hilo lililowakumba wananchi hao.
Katika
salamu hizo, Dkt. Mwinyi amesema kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kupitia Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar iliyopo
katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais itafanya tathmini ya tukio hilo
ili iweze kujua hasara halisi iliyojitokeza ili kuweza kuwafariji
wananchi waliofikwa na maafa hayo.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa
Kaskazini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud upepo mkali ulitokea katika
vijiji vya Kendwa na Nungwi Shehia ya Kiungani, Mkoa wa Kaskazini Unguja
na kusababisha maafa kwa nyumba zipatazo 36.
Rais Dk. Mwinyi amewasihi na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu wananchi wote waliopatwa na maafa hayo kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu.
No comments:
Post a Comment