MAKAMU wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango
leo Machi 23, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na watumishi wa Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, mazungumzo yaliofanyika ofisi
ya wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
Katika
mazungumzo hayo Makamu wa Rais alipokea changamoto mbalimbali
zinazowakabili watumishi hao pamoja mapendekezo na maoni ya watumishi ya
namna bora ya kutekeleza majukumu ya wizara hiyo yenye dhamana ya
kusimamia masuala ya Muungano na Mazingira hapa nchini.
Akizungumza
na watumishi hao, Makamu wa Rais amewataka kufanya kazi kwa bidii,
nidhamu pamoja na kufuata kanuni na maadili ya Utumishi wa umma wakati
wote wanapotekeleza majukumu yao. Aidha amewataka kuwa na ushirikiano na
Ofisi pamoja na Wizara zingine ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
zaidi.
Amesema,
wajibu wa wizara hiyo ni kuhakikisha inalinda na kudumisha Muungano
hivyo amewataka watumishi hao kuratibu vikao vya kamati ya pamoja vyote
kama ilivyopangwa na kutatua changamoto zinazojitokeza pamoja na
kuimarisha yale mazuri yote yanayohusu Muungano.
Ameiagiza
wizara hiyo kuhakikisha inaongeza kasi ya utoaji elimu ya Muungano
kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu, kwa watumishi wa serikali
pamoja na jamii kwa ujumla.
Amesema,
jamii inapaswa kutambua sifa nzuri za Muungano na kuitaka wizara
kutumia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii pamoja na sanaa.
Pia
amewataka watumishi wa Idara ya Mazingira kuhakikisha wanasimamia
kikamilifu suala la mazingira ikiwemo upandaji miti pamoja na usafi wa
mazingira.
Amesema,matatizo
kama yaliojitokeza mto Mara hivi karibuni na kusababisha vifo vya
viumbe hai katika mto huo yanapswa kutambulika mapema kufuatia
ufuatiliaji wa karibu wa mazingira.
Amewataka
watumishi wa wizara hiyo kuwa wa mfano katika suala la upandaji miti na
kuwataka kuchukua hatua binafsi za utunzaji mazingira katika maeneo
wanayoishi.
Pia
Makamu wa Rais amewataka kuendelea kufuatilia maazimio ya kimataifa
pamoja kuongeza ushirikiano na wadau wa mazingira, sekta binafsi,
taasisi za kimataifa , dini pamoja na taasisi za fedha ili kupata
teknolojia rahisi pamoja na upatikanaji wa fedha utakaowezesha
kutekeleza program mbalimbali za mazingira.
Awali
akimkaribisha Makamu wa Rais kuzungumza na watumishi hao, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo
amesema wizara itaendelea kuwa kioo katika suala la muungano na ajenda
ya utunzaji mazingira pamoja na na tayari mafanikio yameanza kuonekana
ikiwemo wananchi mbalimbali kuanza uuzaji na upandaji wa miti katika
maeneo yao
No comments:
Post a Comment