RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali
Mwinyi amesema kuwa ujio wa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea
Duniani (FINA) hapa Zanzibar utasaidia kwa kiasi kikubwa kuitangaza
Zanzibar kiutalii hasa katika utalii wa michezo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali
Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum ya Jahazi na mgeni wake Rais wa
Shirikisho la Mchezo wa Kuogolea Duniani (FINA), Bw.Husain Al Musallam,
baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu
Jijini Zanzibar leo Machi 15,2022.(Picha na Ikulu).
Rais
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo alipokutana na Rais wa Shirikisho la
Mchezo wa Kuogelea Duniani (FINA), Hussain Al Musallam akiwa na ujumbe
wake wa viongozi mbalimbali wa shirikisho hilo kutoka ndani na nje ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwemo waliotoka makao makuu ya FINA
nchini Switzerland.
Katika
mazungumzo hayo Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa mchezo huo ni maarufu
duniani na ujio wa kiongozi huyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha
uhusiano na ushirikiano kati ya Zanzibar na shirikisho hilo la mchezo wa
kuogelea duniani.
Ameongeza
kuwa, hatua hiyo itaisaidia sana Zanzibar ambayo imezungukwa na bahari,
na kwa vile ipo katika mikakati ya kuimarisha Sera ya Uchumi wa Buluu
ambapo miongoni mwa malengo iliyojiwekea ni kuimarisha sekta ya utalii
kwa kupitia utalii wa michezo.
"Tumefurahishwa
kwa kiasi kikubwa na ujio wa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea
Duniani (FINA), Hussain Al Musallam ambapo kuja kwake hapa Zanzibar
kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya
michezo nchini,"amesema Dkt.Mwinyi.
Aidha,
amesema kuwa ujio wa kiongozi huyo ni mwanzo mzuri wa ushirikiano
katika kukuza sekta ya michezo ikiwemo utalii wa michezo ambao kutokana
na mazingira ya Zanzibar mafanikio makubwa yanaweza kupatikana.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali
Mwinyi akizungumza na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Mchezo wa
Kuogolea Duniani (FINA), Bw.Husain Al Musallam (kulia kwa Rais)
alipofika Ikulu jijini Zanzibar na ujumbe wake kwa mazungumzo
yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo. (Picha na Ikulu).
Rais
Dkt. Mwinyi amesema kuwa, ziara ya kiongozi huyo ni nafasi nzuri kwa
Zanzibar kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya michezo
ambayo hivi sasa imewekewa mikakati maalum.
Ameeleza
haja kwa Zanzibar kuwa mwanachama wa Shirikisho hilo la Mchezo wa
Kuogelea Duniani (FINA), hatua ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa
kujifunza mambo kadhaa kutoka shirikisho hilo ambalo limepata mafanikio
makubwa.
Sambama
na hayo, Rais Dkt. Mwinyi ametumia fursa hiyo kumkaribisha Zanzibar
Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (FINA) Hussain Al
Musallam na kumueleza mikakati na malengo yaliyowekwa na Serikali
anayiongoza katika kuimarisha sekta ya michezo hapa nchini ukiwemo
utalii wa michezo.
Naye
Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (FINA), Hussain Al
Musallam amemueleza Rais Dkt. Mwinyi kwamba kuogelea si mchezo tu bali
ni sehemu ya maisha ambapo vijana walio wengi wamekuwa wakiufuatilia.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali
Mwinyi akizungumza na Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogolea Duniani
(FINA), Bw.Husain Al Musallam (kulia kwa Rais) alipofika Ikulu jijini
Zanzibar na Ujumbe wake kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa
Ikulu leo, na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale
Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu
Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali.(Picha na Ikulu).
Amesema
kuwa, miongoni mwa sababu kubwa ya ziara yake ya kuja Zanzibar ni
pamoja na kuja kumuunga mkono Rais Dkt. Mwinyi katika mikakati yake ya
kuimarisha uchumi kupitia Sera ya Uchumi wa Buluu ambao sekta ya utalii
wa michezo imejikita ndani yake.
Kiongozi
huyo wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (FINA), alimueleza
Rais Dkt. Mwinyi hatua mbalimbali zilizowekwa na shirikisho hilo katika
kuhakikisha inaweka programu mbalimbali za mafunzo ya kuogelea kwa ajili
ya vijana ambapo na vijana wa Zanzibar nao watafaidika.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali
Mwinyi akimkabidhi zawadi maalum ya Mlango wa Zanzibar mgeni wake Rais
wa Shirikisho la Kimataifa la Kuogolea (FINA), Bw.Husain Al Musallam,
baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu
jijini Zanzibar leo.(Picha na Ikulu).
Pamoja
na hayo, Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (FINA),
Hussain Al Musallam alieleza azma ya Shirikisho hilo ya kusaidia
kuimarisha sekta ya utalii hapa Zanzibar hatua ambayo itaweza kuitangaza
Zanzibar kimichezo Kimataifa.
Nao
viongozi katika ujumbe huo walieleza kuvutiwa na mazingira ya Zanzibar
ambayo yanauwezo wa kutoa vipaji kadhaa vya mchezo wa kuogelea sanjari
na kuitangaza Zanzibar kiutalii kwani mchezo huo ni maarufu duniani na
hapa Zanzibar umekuwa ukipendwa na vijana.
No comments:
Post a Comment