Kamati ya Viwanda Biashara na
Mazingira imetembelea katika viwanda vya kuzalisha chanjo za mifugo
nchini ( HESTER Biosciences Africa Ltd ) na kiwanda cha kuunganisha
magari (GFA Vehicle Assemblers) .
Akizungumza wakati wa ziara
hiyo Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza magari cha
GFA Vehicle Assemblers, Ezra Mereng' ameomba Serikali kurekebisha sheria
na kupunguza ushuru ili kuwalinda wawekezaji wazalendo kuweza
kushindana na wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi,Pia aliishauri
serikali kuwaomba waagizaji wa magari (trucks) kuagiza vipuri na kazi ya
uunganishwaji ifanyike hapa nichin kuweza kuokoa fedha za kigeni ambazo
zingetumika kwa kuagiza magari na badala yake kutanua soko la ajira kwa
vujana wetu walioko katika viwanda vya ndani
Kiwand hicho
ambacho kipo katika awamu ya pili ya uzalishaji mpaka sasa kimetengeneza
magari 420 kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji ambapo kazi nyingi
katika kiwanda hicho hufanywa na watanzania waliopata ujuzi kutoka kwa
wataalamu wa Kigeni Kwani kiwanda hicho kina wafanyakazi zaid ya mia
moja na kati yao 95 ni watanzania na 5 ni wageni kutoka nje ya mipaka ya
Tanzania.
Akijibu baadhi ya hoja zilizotolwea na wawekezaji hao
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Ashatu Kijaji aliwatoa hofu
wawekezaji hao na kuwaambia kwamba serikali ya amwamu ya sita ipo karibu
nao na suala la ukatikaji wa umeme ambalo ni miongoni mwa changamoto
zilizowasilishwa, Kijaji alisema serikali ipokatika hatua za kuongeza
vyanzo vya umeme mkubwa ikiwemo mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere
litakuwa mkombozi wa tatizo hilo.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Erick Shigongo
alisema swala la kubadilisha sheria kumlinda mwekezaji wa ndani (local
content) kamati itafikisha bungeni kwani wao ndio wenye mamlaka ya
kutunga sharia hizo ili wawekezaji waweze kushindana katika soko na
wawekezaji wakubwa kutoka nje .
Kamati hiyo ilitembelea viwanda
vya kuzalisha chanjo za mifugo nchini ( HESTER Biosciences Africa Ltd )
na kiwanda cha kuunganisha magari ( GFA Vehicle Assemblers )
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza magari cha GFA Vehicle Assemblers, Ezra Mereng' akizungumza na Kamati ya Viwanda Biashara na Mazingira
Waziri
wa Viwanda Biashara na uwekezaji, Ashatu Kijaji akimsikiliza mtaalamu
wa ufundi Kiwanda cha kutengeneza na kuunganisha magari cha GFA Vehicle
Assemblers, Hamadi Ramadhani wakati kamati ya Bunge ya viwanda Biashara
na Mazingira walipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha mkoani Pwani
jana.
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza magari cha GFA Vehicle Assemblers, Ezra Mereng' akizungumza na kamati
Waziri
wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Ashatu Kijaji akiangalia magari
wakati kamati ya viwanda, biashara na Mazingira ilipofanya ziara katika
kiwanda cha magari cha GFA Vehicle Assemblers Kibaha mkoana Pwani
Waziri
wa Viwanda Biashara na uwekezaji, Ashatu Kijaji akimsikiliza mtaalamu
wa ufundi Kiwanda cha kutengeneza na kuunganisha magari cha GFA Vehicle
Assemblers, Hamadi Ramadhani wakati kamati ya Bunge ya viwanda Biashara
na Mazingira walipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha mkoani Pwani
jana.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Tuesday, March 15, 2022
Home
BIASHARA.
Kamati ya Bunge Viwanda yatembelea Kiwanda cha magari cha GFA Vehicle Assemblers Kibaha
Kamati ya Bunge Viwanda yatembelea Kiwanda cha magari cha GFA Vehicle Assemblers Kibaha
Tags
BIASHARA.#
Share This
About kilole mzee
BIASHARA.
Labels:
BIASHARA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment