WASHEREHESHAJI
wakongwe nchini B12 na Samio love wote kutoka kituo cha Redio cha
EFM na Televisheni ya ETV wamewaongoza wamia ya watu waliohudhuria
Machi 12, 2022 Tamasha la Muziki la Serengeti kucheza nyimbo za
Mwanamuziki nguli nchini Profesa Jay ikiwa ni ishara ya kumuenzi na
kumuombea kwa mwenyezi Mungu ampe heri kwenye maradhi yanayomkabili hivi
sasa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wamemwelezea Profesa Jay kama Mwanamuzi ambaye
ametoa mchango mkubwa kwenye muziki wa kizazi kipya.
Wakati
vikipigwa vibao kadhaa vya Profesa Jay umati wote uliimba kwa hisia
kali nyimbo hizo utadhani ni kwaya iliyofundishwa na mwalimu mmoja.
Kwa
hakika hata kama hajashiriki tamasha la Serengeti moja kwa moja kwenye
uwanja wa Chinangali, historia imeandikwa kwa kuteka mioyo ya watu.
Awali,
siku moja kabla ya tamasha la Serengeti wakati wasanii walipotembelea
Ofisi ya Utamaduni, Sanaa na Michezo eneo la Mtumba jijini Dodoma,
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi aliishukuru Serikali kwa
uamuzi wa kugharimia matibabu na kuwasihi wasanii wito kuendelea
kumwombea.
Mwenyezi Mungu ampe wepesi apone mapema na kurejea katika majukumu yake ya kila siku.
No comments:
Post a Comment