A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, March 13, 2022

KAMA HAMUWEZI KUTUSHANGILIA BASI MSITUZOMEE, NJOENI UWANJANI ILA KAENI KIMYA

 

RAIS wa Heshima wa klabu ya Simba , Mohamed Dewji 'Mo' ametuma Salam Kwa mashabiki wa Yanga ambao ufika kuizomea Simba katika michezo yake ya kimataifa.

Mohamed Dewji ametoa kauli hiyo Kwa uchungu kwenda kwa baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao wameonesha nia ya kwenda Uwanja wa Benjamin Mkapa jumapili hii huku lengo lao likiwa ni kuizomea Simba inapokosea.

"Linapokuja suala la kimataifa, Yanga akicheza na timu yoyote, mimi huwa naiombea dua njema Yanga ifanikiwe kwasababu mafanikio hayatokuwa ya Yanga tu bali ni ya Tanzania kwa ujumla" - @Mohamed Dewji

"Niliumia sana kuona Biashara United imeshindwa kusafiri kwenda Libya kwenye mechi yake ya kimataifa" alisisitiza Mohamed Dewji.

Simba inashuka Dimbani kesho Jumapili kuivaa RS Berkane ya Morocco katika mchezo wa raundi ya pili ya makundi katika kombe la shirikisho barani Afrika.

Simba ndio Timu pekee Kwa ukanda wa Afrika Mashariki (Cecafa) ambayo imebaki katika mashindano makubwa barani Afrika .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages