A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 12, 2022

NEMC yang'ara Kimataifa maonesho ya kilimo na mazingira

 

SERIKALI ya Tanzania ni miongoni mwa nchi 130 zilizoweza kushiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira ambayo huwa yanafanyika kila mwaka na kwa mwaka huu yanafanyika kuanzia tarehe 10 hadi 14 Machi, 2022 katika jiji la Doha nchini Qatar.
Aidha, maonesho haya yamejumuisha kampuni za Kimataifa 300, wakulima 100 pamoja na wawasilisha mada wapatao 56 kutoka mataifa mbalimbali.

Maonesho yalifunguliwa Machi 10, 2022 na Waziri wa Wizara ya Manispaa na Mazingira ( Ministry of Municipality and Environment), Mhe. Abdulla bin Abdulaziz bin Turki Al Subaiel.

Lengo kuu la maonesho haya ni kutoa fursa kwa washiriki kuonesha bidhaa na huduma zinazohusiana na kilimo na mazingira.
Meneja Kanda ya Ziwa Victoria, Bw.Jarome Kayombo wakibadilishana uzoefu wa teknolojia ya uhifadhi wa taka zitokanazo na mabaki ya chakula ( food waste) kwenda kutengeneza mbolea. Ameahidi kushirikiana na NEMC kwa kuleta teknolojia hiyo mbadala nchini Tanzania.

Pia maonesho haya yanawapa fursa washiriki kubadilishana uzoefu, technologia pamoja kutafuta masoko na fursa na uwekezaji katika kilimo na usimamizi wa mazingira.

Baraza la Taifa la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ni miongoni mwa taasisi 19 zilizoshiriki kutoka Tanzania.

Tanzania tulikuwa na jumla ya mabanda 19 ambapo kati yake 17 ni kutoka taasisi za Serikali zinazoshughulika na Mazingira, Kilimo, Ufugaji na Uwekezaji.Mhandisi Jane Kadoda ambaye ni Afisa Mazingira Mwandamizi akitoa elimu juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na NEMC kwenye maonesho Kimataifa ya Kilimo na Mazingira nchini Qatar.

Baadhi ya taasisi za Serikali ni pamoja na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania -Qatar, NEMC, TIC, Bodi ya Korosho, Bodi ya Maziwa, Bodi ya Chai, Bodi ya Kahawa, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanyangiko pamoja na Umoja wa Kilimo cha Mbogamboga.

Washiriki wengine kutoka Tanzania ni pamoja na MamboJambo Design, Dumas African, Greencom African Ltd, Natural Shine Traders na Kampuni ya Oasisi Import Export Ltd.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira liliwakilishwa na Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma, Bi. Irene John, Meneja wa Kanda ya Ziwa, Bw. Jarome Kayombo pamoja na Mhandisi Jane Kadoda kutoka Kanda ya Morogoro Rufiji.Washiriki kutoka NEMC wakijadili baadhi ya maoni na mapendekezo yaliyotolewa na washiriki mbalimbali waliotembea banda la NEMC nchini Qatar.

Miongoni mwa wageni waliotembelea banda la NEMC siku ya ufunguzi ni pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Balozi Mahadhi Juma, Balozi wa Burundi – Qatar, taasisi za Serikali, Wizara na Kampuni mbalimbali kutoka nchi washiriki kama vile Wizara ya Manispaa na Mazingira, Kitengo cha Hifadhi ya Bahari wakiwakilishwa na Prof. John Man Kon Wong, Kampuni ya CITC wanaojihusisha na ufungaji mitambo ya kupunguza hewa ukaa kwenye magari, teknolojia ya kuongeza tija kwenye kilimo na mazingira.

Kampuni ya Royal Link hawa wanajihusisha na Uzalishaji na Usambazaji wa Chemikali za Viwandani, Kampuni za kusafisha maji taka na maji ya Bahari.

Aidha, mwananchi mmoja mmoja kutoka Qatar na nchi mbalimbali walitembelea banda la NEMC ili kupata elimu pamoja ma kuelezwa fursa za uwekezaji kwenye mazingira, utalii na kilimo.

Akizungumza katika maonesho hayo , Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Bi. Irene John amesema, maonesho hayo yatafungua fursa nyingi za uwekezaji katika bidhaa na huduma kwani kupitia mawasilisho yaliyofanywa siku ya ufunguzi tarehe 10 Machi, 2022 NEMC imeonesha jinsi gani mazingira ya uwekezaji yameboreshwa kupitia mifumo mbalimbali ya kielektroniki kama vile mchakato wa utoaji vibali vya Tathimini ya Athari kwa Mazingira ( TAM) na pia mfumo wa upatikanaji wa vibali vya taka hatarishi ambao uko katika hatua za mwisho kukamilika.

Kupitia Meneja wa Kanda ya Ziwa, Bw. Jarome Kayombo amebainisha kuwa moja ya faida kubwa kwa NEMC kushiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Mazingira na Kilimo ni pamoja na kuitangaza NEMC na pia kutoa elimu juu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa uwekezaji endelevu.

Aidha, maonesho yametoa fursa ya fursa za uwekezaji na kuelemisha washiriki juu ya mchakato wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira Nchini Tanzania.

Pia maonesho haya yametoa fursa ya kubadilishana uzoefu wa technologia mbadala za kutunza mazingira zitakazoleta tija katika kuboresha maisha ya kila siku.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages