***********************
Na. John Mapepele
Wizara
ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, leo Machi 18, 2022 imemtunukia tuzo ya
heshima ya Kiswahili, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar
wakati alipokuwa akifunga Kongamano la Pili la Idhaa ya Kiswahili jijini
Arusha.
Tuzo hiyo ya heshima ya kutambua mchango wake katika
kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili iliyokabidhiwa na Waziri wa
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya
Serikali.
Kwa upande wake Mhe. Rais Mwinyi ameishukuru Serikali
kwa kumtunukia tuzo hiyo na kueleza kuwa atampatia ari zaidi ya
kuendelea kukitangaza Kiswahili duniani.
Aidha, ametoa wito kwa
Kamati ya Maandalizi kufikiria kufanyia Kongamano la tatu mwakani
Zanzibar ili kuleta maana zaidi ya kueneza na kuendeleza Kiswahili.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na takribani washiriki 200 kutoka idhaa mbalimbali za Kiswahili duniani.
Akimkaribisha
Mhe. Rais, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed
Mchengerwa ameiomba Serikali kuweka vituo vya Utamaduni kwenye Balozi za
Tanzania nje ya nchi ili kukuza na kuendeleza Kiswahili.
Katika
Kongamano hili Mhe. Rais Mwinyi alipata fursa ya kuzindua mfumo wa
kufundisha Kiswahili pamoja na kutoa vyeti vya kuwatambua washiriki na
wadhamini.
Kongamano hili limerushwa mbashara na TBC, ZBC na vituo kadhaa vya Redio na televisheni
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, March 18, 2022
RAIS MWINYI ATUNUKIWA TUZO YA KISWAHILI NA WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO.
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment