*******************
Na. WAF – Dar es Salaam
Waziri
wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kufikia Julai Mosi 2022 Hospitali ya
Mlonganzila ianze kujitegemea yenyewe badala ya kuendelea kuwa chini ya
Bodi ya wakurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili.
Waziri Ummy
amesema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Hospitali ya
Mloganzila wakiwemo wakurugenzi na viongozi waandamizi mara baada ya
kuzindua miradi ya mtambo wa kuzalisha hewa tiba (Oxygen generating
plant) pamoja na mradi wa kuboresha huduma ya mama na mtoto ambao
umelenga kukarabati wodi ya watoto wachanga mahututi (Neonatal ICU).
“Hospital
hii imekuwa chini ya Bodi ya wakurugenzi wa hospitali ya Muhimbili kwa
muda wa miaka minne sasa inatosha ikajitegemee yenyewe, ijisimamie kwa
kujiendesha na kutoa huduma za matibabu kwa wananchi”. Amesema Waziri
Ummy.
Ameongeza kuwa atahakikisha mchakato wa Hospitali hiyo kujitegemea unaharakishwa ili usiweze kukwamisha ifikapo Julai mosi.
Kwa
upande wa uzinduzi wa miradi, Waziri Ummy amesema Mradi wa hewa tiba ya
Oksijeni utasaidia kuzalisha mitungi 200 kwa siku na mradi wa pili
umelenga kukarabati wodi ya watoto wachanga mahututi (Neonatal ICU) kwa
msaada wa Serikali ya Korea.
Aidha, Waziri Ummy amebainisha kuwa
Serikali imeamua kuanza kufanya uwekezaji kwa kusimika mitambo ya
uzalishaji wa gesi tiba baada ya kuona changamoto za upatikanaji wake
pamoja na gharama kuwa kubwa.
“Mwaka 2021 tumefanikiwa kufunga
mitambo Saba katika Hospitali za Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Amana, Geita,
Mbeya, Manyara na Dodoma ambayo imeunganishwa moja kwa moja mpaka wodini
aliko mgonjwa”. Amesema Waziri Ummy
Hata hivyo Waziri Ummy
amesema Serikali ipo mbioni kukamilisha awamu ya pili ya ununuzi wa
mitambo hiyo katika Mikoa kumi na mbili (12) kwa hospital za Rufaa
ikiwemo Njombe, Songwe, Rukwa, Tabora, Kigoma, Mara, Simiyu, Morogoro
Sokoine, Shinyanga, Katavi na Sekoe Toure.
Kwa upande wake Balozi
wa Korea nchini Tanzania Mhe. Kim Sun Pyo amesema nchi yake itaendelea
kutoa ushirikiano kwa Tanzania hasa katika sekta ya Afya na kuahidi
kusaidia katika maeneo yenye uhitaji mkubwa.
“Nchi ya Tanzania na
Korea ilianza ushirikiano muda mrefu toka miaka ya 1992 kwa kusaidiana
katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya na tutaendelea kufanya
hivyo”. Amesema Balozi Kim.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, March 18, 2022
WAZIRI UMMY ATAKA HOSPITALI YA MLOGANZILA KUANZA KUJITEGEMEA
Tags
LOCAL#
Share This
About kilole mzee
LOCAL
Labels:
LOCAL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment