KAMATI
ya Siasa Mkoa wa Singida imeendelea na ziara ya kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo huku ikitoa rai kwa wananchi kujitokeza na
kushiriki kikamilifu katika kazi za maendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa Machi 17, 2022 na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba wakati wa ziara ya Kamati ya
Siasa Mkoa, inayoendelea kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani
Singida.
Alhaji Juma Kilimba amewaeleza wananchi wa Kijiji cha Mwasutianga katika Kata ya Irisya wilayani Ikungi kuwa, miradi yote inayotekelezwa mkoani Singida ni yao.
"Na hii miradi si ya viongozi, kwa hiyo hamna budi kushirikiana na Serikali ili kazi ziendelee kufanyika kwa haraka na kwa ufanisi,"amesema.
Wito
huo ameutoa baada ya kuwakuta wananchi wakiendelea kufanya kazi katika
Mradi wa Kituo cha Afya kinachojengwa Irisya ambapo kinatarajiwa
kikikamilika kitaweza kuhudumia wakazi 30,000 katika maeneo hayo.
Amesema
kuwa, amejiridhisha na ujenzi unaoendelea katika Kituo cha Afya Irisya
kwa kuona utendaji kazi unaendelea na kuona watu wengi wanaojitokeza
kufanya kazi na usimamizi unaoendelea katika mradi huo.
Majengo ya Shule ya Msingi Kintandaa.
Mkurugenzi na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.
No comments:
Post a Comment