NAIBU
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi
Kundo Mathew (Mb) amewataka wakazi maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya
Bariadi kushiriki kikamilfu katika zoezi utekelezaji mfumo wa Anuani za
Makazi pamoja na Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwezi Agosti,
2022.
Mheshimiwa
Mhandisi Kundo ameyasema hayo Machi 10, 2022 wilayani ya Bariadi Mkoa
wa Simiyu alipofanya ziara katika vijiji mbalimbali vya Wilayani humo ya
kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa Anuani za Makazi naotakiwa
kukamiliza ifikapo mwezi Mei 2022.
Alisema
kuwa, wananchi wote wanaoshi katika Wilaya ya Bariadi wakashiriki
kikamilifu katika utekelezaji mfumo wa Anwani za Makazi ili ukawe rahisi
kwenda kutekeleza zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalofanyika
mwezi Agosti, 2022 ambalo litapelekea urahisi wa ufikishwaji wa huduma
na maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo kuendana na idadi yao.
Nae
Mkurugenzi wa Huduma za Posta wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari, Caroline Kanuti alitumia fursa hiyo kuwaelezea
wakazi wa Bariadi umuhimu wa mfumo wa Anuani za makazi
endapo watashiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
“Pale ulipo unaweza ukapata tatizo, unauguliwa au nyumba imewaka moto au kuna mgonjwa anataka kupelekwa hospitali
unapiga
simu unajitambulisha tu kwamba nipo kitongoji fulani unataja na namba
ya nyumba yako kisha yule unaempigia simu atakuja mapka pale ulipo
kwahiyo kupitia mfumo wa Anwani za makazi inakuwa rahisi kupata
msaada,”amesema.
Alisema
kuwa, mfumo wa Anwani za Makazi unarahisisha shughuli za mbalimbali
ikiwemo za kilimo kwa kununua mazao au pembejeo za kilimo popote ulipo
na bidhaa yako kukufikia kwa urahisi
No comments:
Post a Comment