A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 12, 2022

Huduma za ustawi wa jamii kutolewa bure kwa wananchi

 

KATIKA kuadhimisha kilele cha Siku ya Ustawi wa Jamii Duniani yenye kauli mbiu “Juhudi jumuishi dhidi ya ukatili wa aina zote kwa maendeleo endelevu” Taasisi ya Ustawi wa Jamii ikishirikiana na Chama cha watoa huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) na Umoja wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Ulinzi na Huduma za Ustawi wa Jamii (TaCosWe) na wadau wengine watatoa huduma za ustawi wa jamii bure kwa wananchi wote siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani Machi 15,2022 na kuendelea.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt.Joyce Nyoni,amesema ni mwaka wa 15 sasa wanaadhimisha Siku ya Ustawi Duniani kote tangu ilipoanza kuadhimishwa mwaka 2007.
Amesema, ili kuiishi kauli mbiu ya mwaka huu taasisi na wadau watatoa huduma ya ushauri wa masuala ya ndoa na mahusiano, masuala ya watoto waliotelekezwa na ushauri wa kisaikolojia na nyingine nyingi pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu hasa nini maana ya Ustawi wa Jamii na wawatumie vipi wataalam hao kutatua changamoto za kila siku kwenye maisha.

"Nawakaribisha wananchi wote kupata huduma za jamii na elimu zitakazotolewa bure katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii,"amesema.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO),Dkt. Mariana Makuu amesema, “Sababu kubwa ya ukatili unaoendelea hapa nchini ni afya ya akili, tunawakaribisha wananchi wote waje waongee na wataalamu ambao watawasaidia kutatua matatizo yao,”amesema.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa mashirika yasio ya kiserikali ya ulinzi na huduma za jamii,Bi. Hilda Ngaja amesema, "Tunashirikiana na Serikali na wadau wengine katika kustawisha jamii yetu na kuondoa tatizo hili la ukatili linaloendelea nchini kwetu,"amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages