KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio ambaye pia ni Mlezi wa Mfuko wa Faraja ameagiza uongozi wa mfuko wa faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuzingatia katiba na mwongozi wa mfuko huo kwenye ukusanyaji wa mapato, matumizi ya fedha za mfuko huo na huduma kwa wanachama wake.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Christopher Kadio ambaye pia
ni Mlezi wa Mfuko wa Faraja akizindua Mfuko wa Faraja wa Wafanyakazi wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma.
Akizungumza
na uongozi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
amewaelekeza kuingiza mchango wa mwajiri kwenye bajeti ya Wizara kwa
Mwaka 2022/23 ili kuhudumua wanachama wa mfuko huo. Pia amewaagiza
kufanya uchaguzi wa Uongozi wa kudumu wa mfuko ndani ya mwaka huu wa
fedha.
"Mimi
kama Mlezi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
nawasisitiza kuzingatia katiba na mwongozo wa Mfuko hii pamoja na
kuingiza mchango wa nwajiri kwenye bajeti ya wizara," amesema.
Christopher
Kadio alisema hayo leo Machi 11, 2022 kwenye uzinduzi wa Mfuko wa
Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi uliofanyika katika ukumbu wa
Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto, jijini Dodoma.
Aidha,
amewashauri watendaji na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
kujiunga na Mfuko huo kwani faida zake ni nyingi na utawawezesha
wafanyakazi kiuchumi na kuongeza tija kwenye majukumu yao.
Katibu
Mkuu Christopher Kadio amesema kwamba Mfuko wa Faraja wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi ni kama sehemu ya bima ya dharura na kwamba
utasaidia kupunguza msongo wa mawazo wa changamoto za masuala ya dharura
ya kijamii kama kuuguliwa na kufiwa.
“Licha
ya kwamba kujiunga na Mfuko ni hairi ya mtu,lakini kwa faida
nilizozieleza ni ushauri wangu kuwa watu wote wajiunge kwa kuzingatia
faida nilizozieleza, Umojani nguvu na utengano ni udhaifu,"amesema.
No comments:
Post a Comment