Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema serikali ya awamu ya
sita inaendelea kushughulikia changamoto za wazee hasa katika sekta ya
afya pamoja na ulipaji wa mafao kwa wazee hapa nchini.
Makamu wa
Rais amesema hayo alipozungumza na wazee pamoja na viongozi wa dini wa
Mkoa wa Kagera ambapo amewahakikishia kuimarishwa kwa madawati ya wazee
pamoja na serikali kuanza mchakato wa bima za afya zitakazoondoa
changamoto za upatikanaji wa huduma za afya kwa wazee zilizopo hivi
sasa.
Makamu wa Rais amewaasa wazee hao pamoja na viongozi wa
dini kuendelea kudumisha amani iliopo hapa nchini ikiwa pamoja na
kutatua kwa amani migogoro iliopo katika jamii. Amesema wazee wanapswa
kuendeleza mila na desturi za nchi hii ili kukabiliana na mmomonyoko wa
maadili miongoni mwa vijana. Aidha amewaomba viongozi wa dini kuendelea
kuliombea taifa pamoja na viongozi wake ili waweze kupata hekima ya
Mungu katika kuwatumikia wananchi.
Kwa upande wao wazee wa mkoa
wa Kagera wamemueleza Makamu wa Rais changamoto zinazoukabili mkoa huo
ikiwemo kukosekana kwa maadili kwa baadhi ya watendaji wanaosimamia
sekta uvuvi hivyo kufanya sekta hiyo kurudi nyuma. Aidha wamesema
umefika wakati wa mkoa wa Kagera kupata chuo cha ufundi kitakachosaidia
kuinua uchumi wa mkoa huo unaoonekana kukwama kwa muda mrefu.
Halikadhalika
wazee hao wamemuiomba serikali kuwaandaa wananchi wa mkoa wa Kagera
katika kutumia fursa za kiuchumi ikiwemo ya mradi mkubwa wa Kabanga
Nikel utakaotekelezwa katika mkoa huo. Wamsema serikali inapaswa
kuusaidia mkoa huo katika kuinua kilimo kutokana na shughuli hiyo muhimu
ya kiuchumi kufanyika chini ya kiwango kwa muda mrefu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na wazee wa Mkoa wa Kagera wakati akiwa ziarani katika Mkoa huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akisalimiana na wazee wa Mkoa wa Kagera mara baada ya mazungumzo aliyoyafanya na wazee hao akiwa ziarani katika mkoa huo.
No comments:
Post a Comment