Wakurugenzi wa Halmashauri Nchini
wametakiwa kutenga fedha zitokonazo na faida ya miradi ya kupanga,
kupima na kumilikisha ardhi kuboresha ofisi za Maafisa Ardhi pamoja na
kuwanunulia vifaa vya kisasa vitakavyosaidia kuaharakisha zoezi la
kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa ufanisi zaidi tofauti na sasa.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametoa agizo hilo kwa
wakurugenzi hao leo mara baada Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi
Maliasili na Utalii kupokea taarifa ya miradi ya kupanga, kupima na
kumilikisha ardhi katika Halmashauri ya mji Bunda.
Halmashauri
ya mji wa Bunda inatekeleza mradi huo katika vijiji tisa ambapo
inakusudia kupima, kupanga na kumilikisha viwanja 7,450 baada ya kupokea
mkopo wa Shilingi M.400.9 zinazotolewa na serikali kupitia Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Naibu Waziri Kikwete
aliongeza kuwa baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri wanawathamini
Maafisa Ardhi wanapokuwa na fedha za miradi lakini miradi hiyo ikiisha
wanawaweka kando ndio maana ofisi nyingi za maafisa hao ziko katika hali
mbaya.
Naibu Waziri huyo pia aliungwa mkono na Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Bw. Ally Makoa ambaye alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Bunda Emmanuel Mkongo kuboresha Ofisi ya Maafisa ardhi kwa kutumia
sehemu ya faida itakayopatikana kwenye mauzo ya viwanja mara baada ya
kurejesha mkopo kwa Wizara ya Ardhi.
Ripoti ya mradi wa Kupanga,
kupima na kumilikisha ardhi iliyotolewa na Mkurugenzi Halmashauri Mji
Bunda Emmanuel Mkungo inasema bada ya kukamilisha zoezi hili inakusudia
kukusanya Bil. 1.9 zitakazo tokana na mauzo ya viwanja hivyo.
Kufuatia
makadilio hayo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Munge Ally Makoa akaishauri
Halmashauri hiyo na nyingine zenye miradi kama hiyo kutumia sehemu ya
faida hiyo kununua vitendea kazi vya maafisa ardhi na kuboresha
miundombinu ya Ofisi zao.
‘’Haiwezekani kwa wanaokuletea kiasi
hicho cha fedha kufanya kazi katika mazingira magumu wakati ofisi yako
inatoa kipaumbele katika maeneo mengine.’’ Alisema Ally Makoa Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Mali Asili na Utalii.
Mradi
wa Kupanga, kupima na kumilikisha ardhi unaotekelezwa na Halmashauri
Mji Bunda unafanyika katika vijiji tisa vya Mbugani viwanja 650,Shuleni
viwanja 600,Katoriki viwanja 1,000, Ruselu viwanja 700, Kilimani 800,
Zanziba 300, Balili 1, 200, Idara ya maji 2000 na Guta viwanja 200.
Halmashauri ya mji Bunda inatekeleza zoezi la Kupanga, Kupima na
Kumilikisha ardhi katika vijiji hivyo na tayari imeishatumia takriban M.
100 kwa zoezi linaloendelea na Serikali kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi tayari imeisha toa Sh. Bil.50 kukopesha
Halmashauri 55 nchini ikiwemo Chuo cha Ardhi Morogoro, Dar es Salaam na
Tabora.
1. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akikagua vigingi vinavyotengenezwa na Halmashauri ya mji Bunda vitakavyotumika katika Mradi wa kupanga,kupima na kumilikisha ardhi.
1. Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akitoa zawadi kwa Bi.Joyce Nyangoji baada ya kufuraishwa na namna anavyoweza kupanga vigingi kwa ustadi wakati wa ukaguzi wa zoezi la kujenga vigingi vinavyotengenezwa na Halmashauri ya mji Bunda vitakavyotumika katika Mradi wa kupanga,kupima na kumilikisha ardhi.
No comments:
Post a Comment