Mwili wa Mtoto wa kike anaekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 11 hadi 13 ambaye jina lake halijatambulika wala anapotoka, umeokotwa ukiwa umenasa kwenye tope katika mto Faheri uliopo mtaa wa Hangoni C mjini Babati.
Hayo yameelezwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Benjamin Kuzaga wakati alipokuwa akizungumza na Wanahabari
Kamanda
kuzaga amesema mpaka sasa mtoto huyo hakuna taarifa walizozipata kuhusu
ndugu au mzazi anayemtafuta na kwamba mwili wake umehifadhiwa katika
chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospital ya mji wa Babati Mrara.
Katika
tukio lingine kamanda Kuzaga amesema watu watatu wamekufa katika
matukio tofauti ikiwemo mwanafunzi mwenye umri wa miaka 10 Siamoi Yona
baada ya kushambuliwa na mnyama Mamba akiwa anaogelea kwenye mto Ruvu
uliopo wilaya ya Simanjiro.
Aidha
amesema katika kijiji cha Dareda kata ya Ayalagaya tarafa ya Bashnet
wilaya ya Babati mkulima wa Bacho B Dareda kati aligundua mabaki ya
mwili wa binadamu ambaye bado hajafahamika, yakiwa katika shamba la
Hando Baso huku ikisadikika kuwa mtu huyo huenda ameliwa na mnyama aina
ya fisi baada ya kulewa pombe.
Taarifa
ya kamanda Kuzaga imeeleza kuwa Machi 16,2022 ndani ya ziwa Babati kata
ya Bagara mtu aliyefahamika kwa jina la Petro (50) mkazi wa kigongoni
alikutwa akiwa amefariki baada ya kushambuliwa na Mnyama Kiboko akifanya
shughuli za uvuvi kwa kutumia Mtumbwi ziwani hapo.
Mwanafunzi wa
darasa la pili Anayeitwa Siamoi yona (10) anayeishi kijiji cha ngage
kata ya Lobosoit (B) wilaya ya simanjiro Mkoa wa Manyara, amefariki
dunia baada ya kushambuliwa na mnyama Mamba wakati akiogelea katika mto
Ruvu uliopo wilayani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari
kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Manyara ACP Benjamine Kuzaga amesema
tukio hilo limetokea siku ya tarehe 13/03/2022 huko katika mto Ruvu.
Aidha
kamanda Kuzaga amesema yapo matukio mengine yaliyotokana na maafa
ambapo yupo mtoto mwingine Binti ambaye hajatambulika kwa majina na umri
wake unakadiriwa kati ya miaka 11 Mpaka 13 ambapo alisobwa na maji
yanayotokana na Mvua zinazoendelea na hatimaye kupoteza maisha.
Pia
tukio jingine ni la mtu Mmoja aliyeuwawa kwa kushambuliwa na boko
katika ziwa Babati wakati akifanya shughuliza za uvuvi katika ziwa hilo,
ambapo tukio hilo limetokea siku ya tarehe 16/03/2022 katika eneo la
kata ya Bangara wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara.
Kamanda Kuzaga
amesema aliyeuwawa na Kiboko ni Petro Elias sabuni (50) mkulima na mkazi
wa kigongoni, ambapo alikutwa akiwa amefariki baada ya kushambuliwa na
Kiboko wakati akifanya shughuli za uvuvi ndani ya ziwa Babati kwa
kutumia Mtubwi wake.
Aidha katika tukio jingine nipamoja na mtu
Mmoja amefariki dunia mara baada ya kushambuliwa na fisi katika sehemu
mbalimbali za mwili wake huku mabaki ya mwili wake yamekutwa katika
shamba la Hando katika kijiji cha Dareda kata ya Ayagala wilayani Babati
mkoa wa Manyara.
Kamanda kuzaga amesema tukio hilo limetokea
siku ya Tarehe 24/02/2022 ambapo January Flavian (56) mkulima wa kijiji
cha Bacho (B) Dareda kati aligundua mabaki ya mwili wa binadamu ambaye
mpaka sasa hajafahamika ambapo mabaki hayo yalikuwa katika shamba la
Hando Baso na inasadikika kuwa mtu Huyo ameliwa na Mnyama aina ya fisi
baada ya kulewa.
Hata hivyo jeshi la polisi Mkoa wa Manyara
limetoa wito kwa wananchi wote kuchukuwa tahadhari juu ya majanga
yanayotokana na Mvua pamoja na mengine ambayo yanaweza kuhepukika ili
kuokoa maisha juu ya majanga hayo.
No comments:
Post a Comment